Mpwa, Truth will set you Free au hebu some hako ka signature kangu hapo chini; my point is, sidhani kama kweli ni akili/hekima kuishi na mtu na kusema kuwa eti unamficha baadhi ya mambo, ngoja nikupe ushauri niliousikia siku moja;
Nilikua mwaka wa nne pale UDSM na tulikua discussion, hapa tulikua watano siku hiyo, Mimi (Male) na Female wanne ila Mmoja alikua ni Mama Mtu mzima flani hivi, Binti mmoja akauliza swali kua jamani hivi kwenye ndoa ni lazima nimwambie mpenzi wangu kila kitu? kisha akamtaja Mama mwingine as a point of reference kwamba yeye nilipomuuliza swali hilo alisema Si Lazima tena ni mwiko kwani eti sie wanaume hatuna dogo, huyu mama mwingine tuliekua nae muda ule pale akamwambia hivi, binti ni vigumu na ujinga kuishi na mtu mnalala kitanda kimoja kisha useme eti hutaki kumwambia mambo yako, maisha ya namna hiyo hayatakupeleka mbali, lakini pia angalieni ni wapi na nani anawashauri.
My Take
Ni lazima kama unaamua kua kwenye ndoa, mweleze mwenzio ukweli kumbuka kadiri unavyotunza uongo ndivyo unavyokosa amani ya moyo na kutokujiamini, jibu ili lipone dawa yake litumbuliwe kisha likamuliwe, litauma but then litapona and life will go on.
Be blessed