pamoja na udhaifu wa noti hizi watanzania nao hawana heshima na pesa. Hawazitunzi.
Unakuta mtu anachukua hela anazisweka kwenye matiti, au maeneo nyeti, huko zinaloa jasho zinakuwa tepetepe unategemea nini?
Au anauza mkaa, hela zote zitapakaa mkaa, kama muuza samaki toooba pesa yote inanuka samaki.
Acha wale ambao hela wanazikunja kunja kiasi kwamba ili zipite kwenye mashine ya kuhesabia hela lazima ufanye kazi ya ziada kuzinyoosha. Sasa hapo zitaacha kuchakaa kweli?
Tutakapojifunza kutunza hela hata hizi mpya zitadumu.