………………kashfa ya kuanguka kwa benki ya meridien biao haikukuwa kashfa pekee kwa dr rashid akiwa gavana wa benki kuu. Mwishoni mwa mwaka 1994, rais mwinyi alifanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri kwa kumteua jakaya kikwete kuwa waziri wa fedha, na kumuondoa kigoma malima (sasa marehemu). Mchakato mzima wa ufilisi wa meridien biao kwenda kwa benki nyingine ya kigeni – stanbic bank ulifanywa chini ya usimamizi wa kikwete na dr rashid na inasemekana haukuwa wa wazi kabisa. Kulitokea minon'gono kwamba milungula ilitembea.
Pili, wakati akiwa bado gavana wa benki kuu, dr rashid alishinikiza serikali kubadilisha kampuni ya uchapaji wa noti zetu kutoka kampuni ya zamani ya uingereza ya thomas de la rue na kuingia mkataba na kampuni ya giesecke & devrient ya ujerumani. Kampuni hiyo ya uingereza imefanya biashara na benki kuu ya tanzania kuanzia 1966 hadi 1996. Sababu za kubadilisha kampuni ya uchapaji wa sarafu hazikuwekwa sawa kwani wengi wanaona kuwa hii ya ujerumani inachapa noti zisizo na ubora kama ilivyokuwa zamani, zinachakaa haraka sana.
Mapungufu haya, pamoja na ripoti katika gazeti la the east african la agosti 13, 2001, kwamba mapema mwaka huo, 2001 benki kuu ililazimika kuziondoa katika mzunguko mamilioni ya noti za sh 1,000/- kutokana na kuchapishwa vibaya na mchapishaji huyo, bado dr rashid aliendelea kuishinikiza serikali kufanya biashara na kampuni hiyo ya ujerumani. Katika mwaka 1994 pekee, kampuni hiyo ilichapisha vibaya noti za tanzania mara nne. Hizi ni zile za viwango vya sh 500/-, 1,000/- na 10,000/-.
Aidha gazeti hilo liliripoti kwamba kampuni hiyo ya ujerumani pia ilikuwa imekataliwa kuchapisha noti za benki ya umoja wa ulaya (european central bank) baada ya kuchapa vibaya noti za euro za thamani ya mabilioni katika tenda iliyokuwa na thamani ya dola za kimarekani milioni 32.
Ilielezwa kuwa katika zabuni hiyo ya mwaka 2001, wakati kampuni ya thomas de la rue ilikubali kuchapisha noti zetu kwa thamani ya dola za kimarekani 33.02 milioni, kampuni hiyo ya ujerumani ilitaka ilipwe dola 49.15 milioni. Hata hivyo hatimaye wajerumani walishinda kunyakuwa zabuni hiyo.
chanzo mwanahalisi