Japo mimi sio mtu wa BOT, ila msiwe na wasiwasi, zililetwa rangi kiwa bado mbichi, inakauka taratibu kila zinavyokaa kwenye mzunguko mpaka vitafikia hazichuji tena.
Karatasi sio ya magome ya miti, ni karatasi ya pamba laini, ikilowa haichaniki kama kitambaa!.
Na hiyo rangi inayochuja, acha tuu ichuje, lakini noti inabaki ikingaa vile vile kama radioctive material!.
Naombeni tusiwe wepesi kulalamika kila kitu, japo naunga mkono kulalamikia genuine issue kama hii, ila pia tuwe tayari kupongeza kwenye jambo zuri, hivyo tuwapongeze BOT kwa Noti Mpya za size ndogo na hazichakachuliki.