Noti mpya hazina ubora?

Noti mpya hazina ubora?

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239
Noti mpya zazua balaa

Ubora wa noti mpya zilizoanza kutumika mwanzoni mwa mwaka huu unatia shaka, baada ya kubainika kuwa baadhi yake zinachuja na kuacha rangi zikilowa maji au jasho.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili umebaini kuwa noti hizo hasa za Sh 5,000 na 10,000 zikikandamizwa au kusuguliwa kwenye karatasi nyeupe hata bila ya kuloweshwa maji au jasho, huacha rangi.

Hali hii imesababisha baadhi ya watu kutilia shaka ubora wake huku wasomi wakitaka serikalki kuwa makini kwa kuwa inaweza kupata hasara kubwa….

…….Ili kuthibitisa malalmiko hayo, Mwananchi Jumapili ilichukuwa noti ya Sh 5,000 na kuisugua kwenye karatasi nyeupe ikaacha rangi ya bluu…..

Habari zaidi katika Mwananchi Jumapili.
 
Hilo jingine laja!! Nchi hii kiboko kweli kweli!!!
 
Wakuu nilieleza hii issue ya hizi noti kabla hata hazijaingia kwenye mzunguko kuwa ni kimeo, watu wakanishambulia hapa jukwaani sana na kusema sijui technolojia ya kisasa. Mmesahau kujaribu kuchana kidogo mwone nini kitatokea.
 
Mkuu Nguli, nasikia zinachanika kirahisi sana pia; nini kifanyike sasa? Serikali izuie mzunguko wa noti hizi mapema?

Hivi hakuna testing kabla ya kupeleka kwenye mzunguko? Wanadhani watanzania ni vilaza kutoangalia ubora wa kitu walicholetewa na wamekilipia hela nyingi kufikia kinaingizwa sokoni?

Nani wanatakiwa kubebeshwa lawama hizi? BoT? Hazina? Serikali kuu?

Bongo tambarare!
 
Tahadhari!!

Ukilipwa noti mpya zikague vizuri.....
Kwa macho yangu nimeshuhudia juzi Ijumaa mtu kalipwa noti hizo za 10,000 mojawapo ikiwa fake!!
yaani wameshazitengeneza wakati hazijamaliza hata mwezi katika mzunguko
!!
 
hakuzisugua??

kikwetenanotimpya.jpg
 
Bongoland: nchi ya kuchakachua! Tunadanganywa mpaka kwenye noti! Nimechukua noti mpya ya Sh. 10,000 na kuisugua kwa kukandamiza kwenye karatasi nyeupe ikaacha rangi. Nimefanya hivyo kwa noti ya zamani, karati imeendelea kuwa nyeupe. Tumeliwa!!
 
Noti mpya zazua balaa

Ubora wa noti mpya zilizoanza kutumika mwanzoni mwa mwaka huu unatia shaka, baada ya kubainika kuwa baadhi yake zinachuja na kuacha rangi zikilowa maji au jasho.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili umebaini kuwa noti hizo hasa za Sh 5,000 na 10,000 zikikandamizwa au kusuguliwa kwenye karatasi nyeupe hata bila ya kuloweshwa maji au jasho, huacha rangi.

Hali hii imesababisha baadhi ya watu kutilia shaka ubora wake huku wasomi wakitaka serikalki kuwa makini kwa kuwa inaweza kupata hasara kubwa….

…….Ili kuthibitisa malalmiko hayo, Mwananchi Jumapili ilichukuwa noti ya Sh 5,000 na kuisugua kwenye karatasi nyeupe ikaacha rangi ya bluu…..

Habari zaidi katika Mwananchi Jumapili.

Ehee! Rais wa kuchakachua... umeme wa kuchakachua... mafuta ya kuchakachua....
Nchi inaenda kombo... kila mtu yuko bussy kuchakachua kitu ili apate ulaji...
 
noti ya zamani ilikuwa ukiikunja2 ukiiweka sehemu inakunjuka yenyewe ila hizi inabaki ivo2, ni kama karatasi vile! na hizo 1000 walisema wameimarisha kwenye kona hata sijaona huo uimara, ngoja nikatest kwenye rangi.
 
Mkuu Nguli, nasikia zinachanika kirahisi sana pia; nini kifanyike sasa? Serikali izuie mzunguko wa noti hizi mapema?

Hivi hakuna testing kabla ya kupeleka kwenye mzunguko? Wanadhani watanzania ni vilaza kutoangalia ubora wa kitu walicholetewa na wamekilipia hela nyingi kufikia kinaingizwa sokoni?

Nani wanatakiwa kubebeshwa lawama hizi? BoT? Hazina? Serikali kuu?

Bongo tambarare!

Zinaacha rangi kwa mfano ukivaa shati jeupe ukaiweka kwenye mfuko wa shati ukiitoa inaacha rangi kwenye shati, yena na hivi kuna joto sasa hivi ndio usiseme kabisaa
 
au kuna ulaji mwingine wamejitengenezea?? si ni shamba la bibi
 
Na hutasikia mtu kawajibishwa.... Wanajua wabongo mchana wanasema usiku wanalala! Kwisha!! Wizi MTUPU!!
 
Tahadhari!!

Ukilipwa noti mpya zikague vizuri.....
Kwa macho yangu nimeshuhudia juzi Ijumaa mtu kalipwa noti hizo za 10,000 mojawapo ikiwa fake!!
yaani wameshazitengeneza wakati hazijamaliza hata mwezi katika mzunguko
!!

Si unajua wabongo lazima wajaribu kitu kipya, tena na hivi walivyokuwa wanajigamba kuwa hauwezi kutoa noti feki kwenye hizi mpya ngoja uje uone mziki wake
 
Back
Top Bottom