Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
Kisukari ni ugonjwa sugu unaoathiri mtu 1 kati ya 10 duniani kote. Husababisha kiwango cha sukari mwilini kuwa juu sana kwa sababu mwili hauzalishi insulini ya kutosha au hauwezi kuitumia insulini vizuri kama unavyopaswa. Dalili za kisukari ni pamoja na:
🚰 Kuhisi kiu kupita kiasi
🚽 Kuenda haja ndogo mara kwa mara kuliko kawaida
👁️ Maono kuwa hafifu
😴 Kuhisi uchovu
📉 Kupungua uzito bila kukusudia
Kisukari cha aina ya 1 hakiwezi kuzuilika. Ni hali ya kinga ambapo mfumo wa kinga ya mwili hujishambulia wenyewe na kuzuia mwili kuzalisha insulini.
Kisukari cha aina ya 2 kinaweza kuzuilika mara nyingi kwa kuzingatia mtindo bora wa maisha kama vile:
✅ Kuhakikisha una uzito wa mwili unaofaa
✅ Kuwa na mazoezi ya mara kwa mara
✅ Kula mlo bora
✅ Kuacha Sigara
🤰 Kisukari cha mimba kinaweza kutokea wakati wa ujauzito na hutokea mwili unaposhindwa kutengeneza insulini ya kutosha, na kusababisha kiwango cha sukari kuongezeka. Kisukari cha mimba kawaida huisha baada ya kujifungua.
Njia bora ya kugundua kisukari mapema ni kufanya vipimo vya afya mara kwa mara na vipimo vya damu na mtoa huduma ya afya. Utambuzi na matibabu ya mapema ni muhimu ili kuepuka madhara ya kisukari.