Kama unahisi wanachofanya EFM/TVE ni fikra za kimsakini utakuwa unachemka...
Mwaka 2013 Lady Jay Dee aliandaa show yake kubwa tu katika ukumbi wa Nyumbani Lounge- Namanga...Ruge na Clouds nao siku hiyohiyo wakaandaa show ya Mwana FA ukumbi wa Makumbusho - Posta kwa lengo la kumkomoa Jide...Hawakufanikiwa kuharibu show ya Jide kwa sababu Jide alipewa support na Profesa Jay, Sir Nature & Wanaume Halisi, Grace Matata, Langa Kileo, M 2 the P, Mr Sugu na Bantu group Band ya Mzee Kalala....Mwana FA yeye alisindikiwa na Mandojo na Domokaya (ambao walipelekwa na Clouds kwa sababu tu walikuwa na beef na Lady Jay dee), Dully Sykes na Kilimanjaro Band ‘wana Njenje’..
Pia kumbuka kwamba kuna kipindi Mr Sugu na Vinega waliandaa tamasha la Antivirus viwanja vya Posta Kijitonyama ...Ruge na Clouds nao wakaandaa lao Leaders...Kijitonyama palifurika na siku hiyo Mbowe, Lissu, Mdee na wabunge wengine wa Chadema walipanda jukwaani...
Iweje leo uwatuhumu Efm/Tve?
Btw; kwenye dunia hii ya soko huria na utandawazi kila mtu/kampuni ana uhuru wa kufanya jambo analoona linafaa mradi tu havunji sheria...Efm/Tve ni vituo ambavyo vinajitangaza katika soko la habari na burudani...Mkakati wanaotumia kujitangaza ni pamoja na kuandaa matamasha ya bure na kutoa zawadi kwa wananchi kwa lengo la kuwavuta wasikilize/kutazama vituo vyao..Angalia matamasha kama Mchizi wangu, Shika ndinga na Muziki mnene au utaratibu wa kurusha matangazo ya moja kwa moja njue ya studio na kukutana na wasikilizaji wao (NJE NDANI)...Udhamini wa BIKO, Coca Cola na Fast Jet unawapa jeuri ya kuyafanya haya matamasha bure....
Sasa hivi EFM wanarusha matangazo yao mikoa ya Dar, Pwani, Mtwara, Mwanza, Mbeya na Tanga wanapatikana na mikoa jirani na hiyo...Muitikio walioupata katika mikoa hiyo ni mkubwa kiasi cha kuwa tishio kwa Clouds ambao matamasha tyao wanatoza viingilio...Umati uliohudhuria uwanja wa Sokoine juzi kwenye tamasha la Muziki mnene ni mkubwa sana sana...
Efm/Tve ni tishio kwa Clouds FM/TV....Clouds inabidi walijue hilo na kujipanga kushindana katika strategies badala ya mafumbo ya Ruge na public sympathy...
Sorry kwa waraka mrefu...
Wakatabahu...
Bala.