November 25 yagombaniwa, Efm/TvE vs Clouds Media

November 25 yagombaniwa, Efm/TvE vs Clouds Media

Unko T

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
200
Reaction score
266
Mtanange huu ulianza hapo jana pale ambapo TvE/Efm walipotoa tangazo la Ssebo kuzungumza leo na Clouds nao wakapandisha Ruge kuzungumza muda uleule wa Watani wao wa Jadi!

Nimepata butwaa kusikia Efm/TvE watakuwa na tamasha la bure 25th Novemba 2017 ambayo ndio siku Fiesta Dar itafanyika.

Haya sie wajuvi wa mambo husema ngoma bado mbichi...mtoto wa miaka 3 na miezi 8 anamvimbishia babu wa miaka 20.

Hii vita ya kichini chini ni tamu sana na itakuza media za nchi kama wote watakuwa na akili ya ushindani!!!!
 
Nawengine tunaweka tamasha la nyimbo za injili( Gospel music Concert ) siku hiyo hiyo, nimesikia kuwa wasambaa watakuwa na ngoma ya mdumange na kiingilio bure kwa wasambaa wote, kama sio msambaa unaingia kwa buku jero
 
Hahaha kama namuona Makonda atakapoitumia fulsa hii kuhakikisha show hizo zote zinaisha saa 6 usiku.Ikumbukwe show zote za zimakiki washa mziki za TVE huwa zinaonyeshwa live na kuisha saa 6 ya usiku .

Msisahau pia alipozima show ya Omario saa 6 club.
 
Yani niende kwenye tamasha la bure nirudi na ngeu???? kwa sisi wapenda burudani na starehe tunapendelea matamasha yenye viingilio tena ikiwezekana bei ikiwa kubwa mana ustaarabu unakuwepo, tunahangaika kutafuta pesa haipaswi kupata mateso wakati wa kuitumia.....wahenga wanasema "bure gharama"
 
Hata kama ni Competition hicho wanachotaka kufanya Efm/TVE ni utoto sasa... Kwa style hii maendeleo nchi hii ngumu sana

Inajulikana Fiesta ni brand ya clouds kwa nini usipange ratiba zako tarehe nyingine kama unahamu ya kutupa tamasha la bure? To me that is so low and pathetic! Kama wao ndio walianza kutangaza tarehe basi clouds wasogeze mbele
 
Usijitoe ufahamu kujisahaulisha hao clouds walipopanga show ya Mwana Fa wakati siku hiyo Ladyjaydee alikuwa na uzinduzi wa albamu yake na wasanii aliowaalika Jide hawakwenda wakaenda show ya clouds
 
Back
Top Bottom