NSSF bila haya wala aibu

mboamboa

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2013
Posts
237
Reaction score
156
Amini usiamini walichokifanya NSSF kitalaaniwa na wengi na sasa ndio tunazidi kuona uozo na uliopo nchini Tanzania.Mtakumbuka mpiganaji wetu Dr.Maseru alivyokuwa mpiganaji akaacha kukaa na kuwahudumia Wamarekani akaamua kurudi nyumbani Tanzania kuja kutusaidia Watanzania wenzake,NSSF wakishirikiana na Serikali hii ya kinafiki wakamfukuza kwenye majengo yao mpaka wakataifisha vitu vyake wakavipiga mnada,Wamarekani ambao ni madaktari wenzake walisikitika sana wakaamua kumsaidia kwa kumnunulia zana nyingine za kazi na kuanza kumjengea hosipitali ya moyo kule vujibweni na ujenzi ulikuwa unakwenda kwa kasi ya ajabu.cha kushangaza wakati ujenzi unaendelea kwa upande wa Serikali na Nssf walikuwa wanaendelea kimpinga ili malengo yake yasitimie kwa sababu walishaona kuwa hiyo hosipitali yake ya moyo itawanyima wakubwa 10% ambao washazoea kutibiwa nje ya nchi,kilichotokea mzee wa watu wakakamshughulikia akaumwa na kutapika damu ndani ya siku 7 akafariki dunia.Unaambiwa wakubwa walifurahi sana hata kwenye msiba hakuna aliyesikia kiongozi wa serikali aliyetoa pole kwa kazi waliyofanya ishatimia.Gazti la jana kama sijakosea ni nipashe limeandika kwamba NSSF wakiwa viwanja vya sabasaba kuwa wako kwenye mchakato wa kufungua hoaipitali ya magonjwa ya moyo kwa ushiriliano na Apollo ya India,kwa mwenye macho uambiwi Tazama hiyo ndiyo Tanzania uijuayo.niwaulize swali la kizushi,Mzee wetu Reginald Mengi kuna kipindi alitanga kujenga hosipitali itakayokuwa inatibu magonjwa ya moyo mkoani kilimanjaro na akasema itaitwa jina mtoto wake ambaye ni marehemu je ile hosipitali iliishia wapi??????? Hii ndiyo bongo wakubwa wamemshikia bango mpaka leo tushaanza kusahauuuuuu. Hiiii nchi ni ovyooooooo
 
Kwahiyo unataka kututhibitishia kuwa kifo cha Dr. Masau kuna mkono wa NSSF na serikali ya ccm?
 

Umeandika kama umepakiwa kwenye bodaboda. Hakuna mpangilio wa hoja na paragraph, mara Dr Masau mara Reginald Mengi mara Appolo Hosp.

Tulia jipange ikiwezekana jamba kidogo relax lete hoja acha kuchekesha.
 
Ni kweli Motie Mengi Memorial Heart Instistute.....sirikali haiwakubali wawekezaji wa ndani kabisa nakumbuka hata ununuzi wa kilimanjaro hotel walimchinjia baharini.
 

hamna kitu kama hiki huu ni uongo usio na ukweli hata chembe
 

Muthie Mengi Memorial Hospital (RIP)
 
Ni kweli Motie Mengi Memorial Heart Instistute.....sirikali haiwakubali wawekezaji wa ndani kabisa nakumbuka hata ununuzi wa kilimanjaro hotel walimchinjia baharini.
si kipindi ilikuwa inajengwa upande wa kushoto kutoka Moshi - Arusha kabla ya mto Karanga!? sijaja siku nyingi huko kujua imefikia wapi
 
Acheni jamani kulalamika bure, huyo Docta Mungu amlaze mahali pema lakini je alikuwa ni Mzungu? huyo Mengi mlieyetaka auziwe Kilimanjaro ni Mzungu? sifa ya kwanza ya mwekezaji tunayemthamini lazima awe Mzungu angalau Muasia.

na kuonesha tuko Serious na wawekezaji wa nje, hatutaki kodi zao. sasa nyie wabongo tunaanza kukata kodi kwa kumiliki laini ya simu. tutafuata kodi ya kumili choo hapana kutumia choo maana wengine tunajua mmepanga

Swali kwenu mtafanya nini? mtabaki kukasirika na kuharibu siku zenu, sisi tunafanya tutakalo. NDIO WENYE NCHI
 
 
si kipindi ilikuwa inajengwa upande wa kushoto kutoka Moshi - Arusha kabla ya mto Karanga!? sijaja siku nyingi huko kujua imefikia wapi

Ilisha anza kujengwa ikacmama kwa muda kutokana na mgogoro leo hi mbele yake kuna sheli kubwa inaitwa panone hi ndo tz.
 
PANONE ndio nani?

Wewe mwekezaji wa kitanzania tatizo lenu hamkati ganji .....hivi mnafikiri sisi tutakula wapi na mishahara midogo na mnatuchunguza movement zetu kila wakati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…