mboamboa
JF-Expert Member
- Jan 30, 2013
- 237
- 156
Amini usiamini walichokifanya NSSF kitalaaniwa na wengi na sasa ndio tunazidi kuona uozo na uliopo nchini Tanzania.Mtakumbuka mpiganaji wetu Dr.Maseru alivyokuwa mpiganaji akaacha kukaa na kuwahudumia Wamarekani akaamua kurudi nyumbani Tanzania kuja kutusaidia Watanzania wenzake,NSSF wakishirikiana na Serikali hii ya kinafiki wakamfukuza kwenye majengo yao mpaka wakataifisha vitu vyake wakavipiga mnada,Wamarekani ambao ni madaktari wenzake walisikitika sana wakaamua kumsaidia kwa kumnunulia zana nyingine za kazi na kuanza kumjengea hosipitali ya moyo kule vujibweni na ujenzi ulikuwa unakwenda kwa kasi ya ajabu.cha kushangaza wakati ujenzi unaendelea kwa upande wa Serikali na Nssf walikuwa wanaendelea kimpinga ili malengo yake yasitimie kwa sababu walishaona kuwa hiyo hosipitali yake ya moyo itawanyima wakubwa 10% ambao washazoea kutibiwa nje ya nchi,kilichotokea mzee wa watu wakakamshughulikia akaumwa na kutapika damu ndani ya siku 7 akafariki dunia.Unaambiwa wakubwa walifurahi sana hata kwenye msiba hakuna aliyesikia kiongozi wa serikali aliyetoa pole kwa kazi waliyofanya ishatimia.Gazti la jana kama sijakosea ni nipashe limeandika kwamba NSSF wakiwa viwanja vya sabasaba kuwa wako kwenye mchakato wa kufungua hoaipitali ya magonjwa ya moyo kwa ushiriliano na Apollo ya India,kwa mwenye macho uambiwi Tazama hiyo ndiyo Tanzania uijuayo.niwaulize swali la kizushi,Mzee wetu Reginald Mengi kuna kipindi alitanga kujenga hosipitali itakayokuwa inatibu magonjwa ya moyo mkoani kilimanjaro na akasema itaitwa jina mtoto wake ambaye ni marehemu je ile hosipitali iliishia wapi??????? Hii ndiyo bongo wakubwa wamemshikia bango mpaka leo tushaanza kusahauuuuuu. Hiiii nchi ni ovyooooooo