Jumatatu niliamua nipite daraja la Kigamboni kuelekea mjini. Nilipofika pale sehemu ya kulipia (Toll Centre) nikaona kuna picha za wanasiasa wawili zimebandikwa kwenye nguzo.
Hizi ni picha za ndugu John Joseph Pombe Magufuli (kwa wasiofahamu huyu ni Mgombea urais kupitia CCM) na ndugu Faustine Ndungulile (mgombea ubunge kupitia CCM).
Nafahamu ile ni ofisi ya umma, je kubandika picha za Wagombea ni sawa?
Je, wakija CUF ama ACT na picha zao nao pia watabandika bila kikwazo chochote?
Naamini uongozi wa NSSF hapo Kigamboni darajani mtanipatia majibu ambayo yanaweza kusaidia vyama vingine pia kuja kubandika picha za wagombea wao kwenye hilo eneo la kulipia.