NSSF kutatua tatizo la umeme Tanzania

NSSF kutatua tatizo la umeme Tanzania

Game Theory

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2006
Posts
8,546
Reaction score
855
Wakati Pension Funds zingine zikiwa hazina Investment Policies zinayoeeleweka, NSSF on the other hand wameamua kwenda Kivyao na sasa wanaingia officially kwenye biashara ya investment ya Kuwa Independent Power Supplier Tanzania.

Pension Funds zingine wamesema kuwa hili jambo wao wao bado ni kubwa mno na hawawezi kufanya maamuzi ya haraka kwani decision making Mechanism zao ni tofauti na NSSF (apparently ndio maneno ya ERIO wa PPF alipoulizwa lini wanaingia kwenye hii biashara)

On the other hand Dr Dau kule NSSF washasema kuwa hawatokaa kusubiri na wameamua ku goa head na mpango wa kutuletea umeme kwani ni AIBU kwa taifa kufikisha miaka 50 huku tuko gizani

For that I congratulate NSSF.


Habari zaidi hapa:

allAfrica.com: Tanzania: NSSF Set to Pour Funds in Electricity Generation


This is the best news na naomba wawezeshwe maana to be honest its impressive na inatia moyo kuona kuwa kuna watu pamoja na matatizo yoote tulionayo kama taifa, bado tunao ma PATRIOTS


 
Hivi hawa kazi yao si ni kuinvest pesa za pensioners na kuzizalisha kwa wingi ili kuwanufaisha pensioners.... kwahiyo kazi yao sio kutoa service bali ni profit oriented....(kuangalia wapi wakiweka pesa itakuwa ina most returns) sasa kweli wamefanya homework na wameshaona return on investment au.....?
 
Hawa NSSF/PPF nitawaelewa kama wataelekeza investment zao kwenye kujenga nyumba za bei nafuu kwa ajili ya watu wa kawaida amabo ndio wateja wao wengi. haya mambo ya kujenga matower sioni kama yana faida kwa stakeholders.

Kwa nini wasitenge bajeti ya kunjenga nyumba japo 50 kila mkoa kila mwaka na kuziuza kwa walimu,polisi na wafanyakazi wengine.

Kama NSSF wanasaka faida hivyo sasa CRDB na EXIM wafanyaje.

Nyumba ni best asset kwa pensioner kuliko pension ya mshiko.

sliding roof said:

This is the best news na naomba wawezeshwe maana to be honest its impressive na inatia moyo kuona kuwa kuna watu pamoja na matatizo yoote tulionayo kama taifa, bado tunao ma PATRIOTS

Mkuu sikubaliani nawe kwa hoja hii kwani Mission ,vision au core business ya NSSF inatakiwa kuwa nini.

Usije ukajikuta unawasifu hata CCM au CDM wakitsema wanaleta mitambo kama hiyo just bcs kuna tatizo la umeme
 
kuna haja ya ile regulatory body kuingilia hii mipango kwani siku haya mashirika yakipata hasara watakaoumia ni sisi tunaochangisha... we will have nothing when we retire/expire

stakeholders involvement is also very important, ni pesa zetu kwa hiyo kila wanapoingia kwenye hizi ventures, our concurrence is vital... what if the venture fail? who will shoulder the loss?
 
kuna haja ya ile regulatory body kuingilia hii mipango kwani siku haya mashirika yakipata hasara watakaoumia ni sisi tunaochangisha... we will have nothing when we retire/expire

stakeholders involvement is also very important, ni pesa zetu kwa hiyo kila wanapoingia kwenye hizi ventures, our concurrence is vital... what if the venture fail? who will shoulder the loss?


Umenena hapo Mkuu. Kutokana na mikataba ya kifisadi kila kona ya nchi yetu stakeholders inabidi wahusishwe katika maamuzi makubwa kama haya ili kuweza kupata idhini yao, vinginevyo management ya NSSF itakuwa inafanya maamuzi ambayo hawana haki ya kuyafanya bila ya kuwashirikisha wenye mali yao.
 
Huu ni wizi mpya unapikwa, kibaya zaidi safari hii wataibiwa wafanyakazi wawekao akiba yao pale na taifa kwa ujumla.
NSSF inatakiwa ikae mbali kabisa na shughuli za kuzarisha nguvu za umeme si kazi yao. Hata kwenye masuala ya Ujenzi wa nyumba na ukodishaji inabidi wajitoe kabisa wao biashara yao ni pesa na si vinginevyo

Si kila mwenye pesa anajiingiza kufanya kila biashara
 
I dont think there is anyone out there who knows whats in NSSF books I have a feeling future governments will have to bail it out ,they are not transparent they are getting ripped off big time in their real estate deals now they wanna get into what?utility please
 
Eti wajenge nyumba zakuuzia polisi na waalimu..lol That is BS and those are not even investments, pensioners will die bila sumni
 
hivi NSSF did they involve members to discuss this, je when business goes bankrupt what will they say? hivi huyu Dau na yeye anaamka tu
na kutoka kwake na kutoa decision, seems one sided, wanachama uliwauliza? hela si zako hizo za wanachama, talk to them, let them
seat down with board members wakikubali na uwezo upo then GO ahead, ila TAHADHARI hakuna mkono/ushauri toka kwa mafisadi
ili mtupooze kwa DOWANS kulipwa, inaonekana kama mnataka kufukia mashimo wakati issue ya Dowans is HOOOT
 
I dont think there is anyone out there who knows whats in NSSF books I have a feeling future governments will have to bail it out ,they are not transparent they are getting ripped off big time in their real estate deals now they wanna get into what?utility please

Afadhali na wewe umeshtuka. Niliuliza ivi posho za wakurugenzi wa nssf ni kiasi gani...hakuna mwenye jibu! Hizi ndo parastatal bodies zetu!
 
Mkuu sikubaliani nawe kwa hoja hii kwani Mission ,vision au core business ya NSSF inatakiwa kuwa nini.
kazi yao inatakuwa kuwa ni mfuko wa Taifa ya hifadhi ya jamii, kwa mujibu wa sheria.

Haya mashiriki ya umma, kila moja, linaanzishwa kwa sheria ya Bunge kwa kazi maalum.

Hizi habari za NSSF kugeuka TANESCO ni uongo mtupu
 
Huko nyuma walisema wangewekeza katika ujenzi wa daraja la Kigamboni. Iliishia wapi? Hili ni changa jingine la macho.
 
Hivi hawa kazi yao si ni kuinvest pesa za pensioners na kuzizalisha kwa wingi ili kuwanufaisha pensioners.... kwahiyo kazi yao sio kutoa service bali ni profit oriented....(kuangalia wapi wakiweka pesa itakuwa ina most returns) sasa kweli wamefanya homework na wameshaona return on investment au.....?

Kufuwa na kusambaza umeme ni investment kubwa inayolipa vizuri sana.

Usione Tanesco invyokufa ukafikiri kuwa si biashara nzuri. Tanesco ni wenyewe wanaofanya madudu, wizi, ubadhirifu ndio unawafikisha pabaya, kama kawaida ya mashirika yote ya uma yaliyokufa.

NSSF huwa wanaingia mikataba na mashirika binafsi na wao huinvest mifedha na huwaachia wenye uzoefu wa mambo hayo kuendesha hizo kazi, na kaka ujuavyo, kila kiwanda au shirika la uma linaposhindwa, likichukuliwa na watu binafsi linashinda.

Nampa pongezi Dau kwa kuiona hii opportunity.
 
Huko nyuma walisema wangewekeza katika ujenzi wa daraja la Kigamboni. Iliishia wapi? Hili ni changa jingine la macho.
Wanaona kuiba kodi zetu haitoshi na sasa wemeamua kuiba na akiba zetu. Grrrrr !
 
wakati pension funds zingine zikiwa hazina investment policies zinayoeeleweka, nssf on the other hand wameamua kwenda kivyao na sasa wanaingia officially kwenye biashara ya investment ya kuwa independent power supplier tanzania .


Pension funds zingine wamesema kuwa hili jambo wao wao bado ni kubwa mno na hawawezi kufanya maamuzi ya haraka kwani decision making mechanism zao ni tofauti na nssf (apparently ndio maneno ya erio wa ppf alipoulizwa lini wanaingia kwenye hii biashara)


on the other hand dr dau kule nssf washasema kuwa hawatokaa kusubiri na wameamua ku goa head na mpango wa kutuletea umeme kwani ni aibu kwa taifa kufikisha miaka 50 huku tuko gizani

for that i congratulate nssf.


Habari zaidi hapa:

allafrica.com: Tanzania: Nssf set to pour funds in electricity generation


this is the best news na naomba wawezeshwe maana to be honest its impressive na inatia moyo kuona kuwa kuna watu pamoja na matatizo yoote tulionayo kama taifa, bado tunao ma patriots



Why now????????? Kuna institution zingine zinachukulia hili suala la umeme dili kwao btwn NSSF wamefanya homework ya kutosha on this project maana wasije wakainvest pesa za pensioners halafu tukasikia habari nyingine. Vile vile suala la Daraja la Kigamboni wameishia wapi maana naona wanaruka form one project to another ili hali hakuna ambacho kimeishafanyika on the previous project ya Daraja la Kigamboni sijui tuwaelewe vipi????
 
Guys

Naomba bora tuliangalie hili suala kwa marefu na Mapana maybe for once tungeacha ushabiki na kuwa walau objective kwenye kujibu au kuchangia hii mada. One would have thought kuwa kijireserach kidogo na hasa from someone who post ina forum that prides it members as GREAT THINKERS angeweza kuliangalia hili kwaupana zaidi. Issues za kutazama hapa ni zi fuatazo:


-Current state ya Umeme Tanzania



-Makosa yaliyofanyika wakati wa liberalisation ya sekta ya Umeme



-Role ya NSSF kwenye hili itakuwa ni ipi?



-Je NSSF wanaruhusiwa na stakeholders wao kuingia kwenye hii biashara yak u generate umeme?



-Je kuna faida yoyote itapatikana kwenda NSSF?



-Je wenzetu wan je wanafanya vipi?


Sasa majibu ya hapa yanaweza yakatoa mwanga walau kiasi mkaelewa why I support hawa jamaa kufanya mambo kama haya.
Umeme Tanzania:


Tanzania mwenye jukumu la generate, transmit and distribution ya umeme zamani ilikuwa exclusively TANESCO ambayo kama mjuavyo ni shirika la umma kwa asilimia 100 na wako responsible kupply asilimia 98 ya umeme Tanzania
Statistics zinasema hivi:

- Megawati 381 za umeme ambao tunatumia sasa hivi unatokana na vyanzo vya maji


-Tanzania tuna uwezo wa kuzalisha mpaka Megawatt 5,000 ya umeme


- Per capita electricity consumption yetu ni 46/KWh per annum, ambayo inakuwa kwa asilimia 11-13 au zaidi


Hiyo ni moja kati ya sababu serikali inataka sana secta binafsi ziingie kwenye haya mambo ya kugenerate umeme. Mind you nchi ina watu milioni 40 na ni LESS THAN 10 % wako connected kwenye umeme. Serikali yetu pamoja na madudu mengi yanayotokea huwa ni competent kwa kujua matatizo ila tatizo huwa ni kwenye namna na njia ya kuyatatua hayo matatizo.

Ndio maana kama mnakumbuka miaka ya 90's waliamua kulegeza masharti na kufanya reform kwenye hii sekta ya nishati na kuruhusu wazalishaji binafsi na hapo ndipo walipoingia the Songas na IPTL kwa nia ya kupunguza shedding, Of course it was not without controversy za akina RUGEMALILA (the same dude aliyeingia ubia na TRITEL) na mwishowe wakapelekana mahakamani, yaani IPTL na TANESCO lakini kujua haya yote inabidi uelewe connection kati ya EastCoast Energy v/s Independent Power Tanzania Limited (IPTL) v/s Songas v/s Ministry of Energy and Minerals (Wizara ya Nishati) v/s Parastatal Sector Reform Commission (PSRC) v/s Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) v/s VIP Engineering Limited (VIP), v/s (TANESCO) v/s NETGroup Solutions vs SIDASida) na bila kuwasahau waheshimiwa wa pale World Bank.



Lakini ukiachilia hao wauzaji wakubwa kulikuwa na wauzaji wengine wadogo kwa TANESCO, kama vile Tanwat (2.5 MW), Kiwira Coal Mine (6.0 MW) na bila kuwasahau Kilombero Sugar (2.5 MW) Mindhali humu kuna GREAT THINKERS nashauri mtafute Economic Recovery Program (ERP) ya 1986-1989 kati yetu na jamaa wa World Bank na IMF ndio mtaelewa kiini cha yoote haya ya reform kwenye sekta hiina zinginezo

MAKOSA TULIYOYAFANYA:



1. POOR COORDINATION: Victim mkubwa hapa alikuwa ni ESI nah ii ilisababishwa na poor coordination. Kupitia wizara mabali mbali (jambo ambalo mpaka leo linaendelea) bilakusahau wadau na wahisani wakati uleee wa kujadili mikataba ya Songas na IPTL. Kama taifa we PAID A HEAVY PRICE. Of course itakuwa ni jambo rahisi sana kukaa hapa na kuanza mambo ya finger pointing lakini haya ndio yale yale kuwa hatutaki kutatua mambo madogo madogo kama ya COORDINATION imagine HAZINA vs NISHATI vs TANESCO vs DONORS vs EVERYONE !!!



2.POOR PRIORITIZATION: Tusijindanganye, evitable consequence of poor coordination is that power sector reforms have been neither clearly prioritized nor implemented na Serikali yetu. Mfano mdogo hatuna clear policy framework for private sector investment katika secta hii, issue skama target percentage of private generation, standard investment incentives and contractual norms kwa jili ya PPA. Bila kusahau kuwa hatuna clear and feasible roadmap for how to make the main off-taker financially and technically viable. Matokeo yake Sekta hii ya Nishati Tanzana in the last 20 years has the sector has gone from dealing with crisis after crisis (kwanza kiangazi cha miaka ya 90 then issue ya high capacity charges, na mengineyo), hii yote imepelekea kudelay of the planning and execution of fundamental reforms necessary for the long-term sustainability of power supply and expansion kwenye nchi yetu na mbaya zaidi hatujui hata priority zetu ziko wapi when it comes to alternative energy!!!! Yaani tumekuwa kama motto mkiwa asiye na baba wala mama wala ndugu wa kumtazama.




3. FAIR AND INDEPENDENT REGULATION: Bila hii hatutofika na hakuna investor atakaye taka kuja kuinvest kwenye hiii sektaka kama hatuna transparency . Imagine kama regulator angekuwepo enzi zile IPTL na Songas wameanza it means akina Mhavile and Co wangekuwa wako bize kuzalisha umeme badala ya kushinda Mahakamani na kwingineko. Sasa hivi tunao EWURA lakini hao wamekuwa kama vile PPRA hawana nguvu zozote zile na sote tunajua no one knows or lets just say its unclear when truly independent oversight will commence. This fact may have cost the country past and present investments and may ultimately impact on future investments.



Sababu zingine ni kutokuwepo kwa uwazi kwenye UNFAIR BIDDING PROCESS, ARBITRATION , CURRENCY DEVALUATION na mengineyo bilakusahau kuwa tunashindwa kua attract makampuni ya uhakika kama TATA kwa kuwa we are not interested na pili hawa washazowe mambo ya transparency sie hayo hatutaki...!



ROLE YA NSSF


Kwenye hili as far as I know NSSF itakuwa ni IPP yaani independent power Producer kama walivyokuwa wengine ila kazi ya distribution ni ya Tanesco hivyo kama wataleta ma generator yao au watatengeza wa Jua au upepo au Gesi toka songo songo thats up to them


JE SHERIA INAWARUHUSU NSSF KUFANYA HIVI:

I would imagine NSSF sio PPF so I cant see them getting involved na jambo ambalo liko kinyume au sheria haiwaruhusu kulifanya. Sina sheria Mama ya ambayo naweza ku quote lakini kama kuna IPP zaidi ya 10 Tanzania sidhani kama wameenda kinyume na sheria. Nadhani hii ipo kwenye investment policy yao so this shouldn't be an issue. Pia si vibaya mkajua kuwa shirika hili lina BOARD ambayo wao ndio wenye maamuzi ya mwisho kwenye mambo kama haya na ndani ya bodi wapo wawakilishi wa wafanyakazi sasa sidhani kama maamuzi yanaweza kufanywa na mtu mmoja

RETURNS:

Kama watu wa investment as far as I know ni kuwa kwa Tanzania inasemekana return ya investment kwenye umeme ni 300% sasa surely hapa naona ni win win situation kwa NSSF


WENZETU NJE WANAFANYAJE?

Malaysia, Philipines,Brazil,Vietnam,India, Jordan, Egypt na kwingineko Pension Funds zao wameinvest kwenye umeme na wanapata returns kubwa sana
Btw TANESCO washankatia umeme ntarudi baadae.
 
Wasiwasi wangu ni dhamira ya hao watu na kitakachotokea huko mbeleni. Mambo huanza hivi baadae unasikia wameingia ubia na hao wanyonyaji viona mbali halafu unasikia wameliwa tena au wanadaiwa mabilioni na huku hela za pensioners zimeondoka. Sijasahau sakata la Manji na majengo yake!
 
Why now????????? Kuna institution zingine zinachukulia hili suala la umeme dili kwao btwn NSSF wamefanya homework ya kutosha on this project maana wasije wakainvest pesa za pensioners halafu tukasikia habari nyingine. Vile vile suala la Daraja la Kigamboni wameishia wapi maana naona wanaruka form one project to another ili hali hakuna ambacho kimeishafanyika on the previous project ya Daraja la Kigamboni sijui tuwaelewe vipi????


Why not now? If not now when?

Daraja as far as I know in few months time contractor atakuwa site

msimsikilize tule waziri anayeitwa POMBE alikuwa ana bwatuka tuuu bila kujua hali halisi...si mmeona kakaa kimya?
 
NSSF Wanafanya hivi kwa shinikizo la wakuu wa nchi na s lingine lolote. Wakuu wanataka wanekane kama wanalifanyia kazi suala la umeme lakini haileti maana kwa mfuko wa pension kuingia kwenye kuzalisha na kusambaza umeme. Wastaafu wataumia saana kama mambo yasipoenda vizuri.
 
Back
Top Bottom