NSSF Kutekeleza Mradi wa Uwekezaji wa Jengo la Ofisi na Jengo la Kitega Uchumi Dodoma

NSSF Kutekeleza Mradi wa Uwekezaji wa Jengo la Ofisi na Jengo la Kitega Uchumi Dodoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

NSSF KUTEKELEZA MRADI WA UWEKEZAJI WA JENGO LA OFISI NA JENGO LA KITEGA UCHUMI DODOMA

*Ni katika eneo la Njedengwa, kujenga hoteli ya nyota 5

*Mkuu wa Mkoa asema uwekezaji huo utachochea uchumi na utalii

Na MWANDISHI WETU,

Dodoma. Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), unatarajia kufanya uwekezaji mkubwa katika Jiji la Dodoma kwa kujenga jengo la minara miwili ambalo litachochea ukuaji wa uchumi na utalii katika jiji hilo.

Habari hiyo njema imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, tarehe 20 Disemba 2024 wakati wa ziara ya kikazi kutembelea mradi huo pamoja na zoezi la kupanda miti katika kiwanja namba 3 kitalu F, kilichopo Njedengwa jijini Dodoma. Ziara hiyo iliyojumuisha Mameneja Wote was NSSF pamoja na Menejimenti ya NSSF ilifanyika mwishoni mwa wiki.

Bw. Mshomba amesema NSSF imeamua kuwekeza katika mradi huo kwa sababu shughuli za uwekezaji ni jambo la msingi na wamekuwa wakiwekeza kwenye maeneo tofauti tofauti ili kuhakikisha thamani ya michango ya wanachama haipotei na kupata faida inayoiwezesha Mfuko kulipa mafao kwa wanachama wake.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameipongeza NSSF kwa mpango wa utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo mkubwa ambao utachochea ukuaji wa uchumi na utalii katika mkoa huo ambao ndio Makao Makuu ya Nchi, utaleta heshima katika Kanda ya Kati na Taifa kwa ujumla.

Mhe. Rosemary amesema Serikali inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali yenye malengo ya kukuza uchumi pamoja na biashara ya utalii na kuwa mikakati hiyo imeanza kuzaa matunda baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuifungua nchi pamoja na kuzindua filamu ya ‘The Royal Tour’ ambayo imechangia ongezeko kubwa la watalii hivyo ujenzi wa kitega uchumi hicho cha NSSF utakuwa chachu ya kuchochea uchumi.

“Mimi ninaposhuhudia NSSF mnakuja kuwekeza mradi mkubwa wa namna hii nawaona ni waelewa wa haraka sana wa kumuelewa Mhe. Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan,” amesema Mhe. Rosemary.

Amesema mojawapo ya vitu ambavyo Rais anatamani kuviona ni kuona Mkoa wa Dodoma ambao ndio Makao Makuu ya Nchi unaleta mikutano ya kimataifa, hivyo ujenzi wa jengo hilo la kitega uchumi la NSSF linaendana na azma ya Serikali ya awamu ya sita ambayo inaendelea kuufungua mkoa huo pamoja na maeneo mengine nchini.

Mhe. Rosemary amesema kukamilika kwa hoteli hiyo pamoja na uwanja wa ndege wa Msalato utachochea shughuli za kiuchumi, kufungua fursa mpya za mikutano ya kimataifa jijini humo, kuongeza mnyororo wa thamani pamoja na kuzalisha ajira.

Ametumia fursa hiyo kuipongeza NSSF kwa kupata mafanikio mbalimbali ambapo hivi sasa thamani ya Mfuko imefikia trilioni 8.5 jambo ambalo limechangiwa na kuwepo kwa ongezeko kubwa la wawekezaji, kukua kwa sekta binafsi na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, amesema utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kuanza mwezi Mei 2025 na utakamilika ndani ya kipindi cha miaka mitatu, ambapo miongoni mwa faida zinazotarajiwa ni kuchochea utalii wa mikutano, kuvutia wawekezaji na kuongeza ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja. Mradi huo unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 148.40 kwa gharama za awali za mradi.

Bw. Mshomba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi ambazo amekuwa akizifanya katika kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini, ambapo kwa upande wa NSSF imepata mafanikio makubwa katika miaka ya hivi karibuni kwa kuongeza wanachama na waajiri pamoja na ongezeko la michango na kusababisha thamani ya Mfuko kufikia trilioni 8.5.

“Mafanikio yote hayo yanatokana na juhudi kubwa ambazo Mheshimiwa Rais wetu amezifanya katika kuboresha mazingira ya uwekezaji, lakini pia juhudi zinazochukuliwa na Bodi ya Wadhamini, Ofisi ya Waziri Mkuu na BoT,” amesema Bw. Mshomba.

Amesema mwezi Juni 2024, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara ya kikazi katika jiji la Mwanza alitembelea mradi wa uwekezaji wa jengo la hoteli ya nyota tano ambapo alishauri NSSF ikipata mapato mazuri zaidi, uiangalie kuwekeza kwenye maeneo mengine ikiwemo mji wa kiserikali Dodoma, hivyo pamoja na kutekeleza mpango wa NSSF kuwekeza Dodoma kwa mujibu wa miongozo na sera za uwekezaji lakini pia ni utekezaji wa maono na maelekezo ya Mhe. Rais.

Awali, akitoa taarifa ya mradi huo, Mhandisi Helmes Pantaleo, Meneja Usimamizi wa Miradi NSSF, amesema mradi huo unatarajiwa kujengwa jengo la ghorofa 16 na kuwa umegawanyika sehemu tatu ikiwemo ya ofisi, hoteli na maduka makubwa.

Mhandisi Pantaleo amesema hoteli hiyo itakuwa na vyumba 120 kikiwemo chenye hadhi ya kulala viongozi wakuu na migahawa mbalimbali.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.30.46.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.30.46.jpeg
    1.1 MB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.30.42.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.30.42.jpeg
    1.2 MB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.30.48 (2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.30.48 (2).jpeg
    1.5 MB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.30.49.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.30.49.jpeg
    1.3 MB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.32.17.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.32.17.jpeg
    1,023 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.32.18.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.32.18.jpeg
    1.1 MB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.32.29.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.32.29.jpeg
    1.3 MB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.32.26.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.32.26.jpeg
    1.1 MB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.32.24.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.32.24.jpeg
    1 MB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.32.23.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.32.23.jpeg
    972.1 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.32.22.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-21 at 07.32.22.jpeg
    706.4 KB · Views: 6
Walitakiwa wahakikishe wanakamilisha kabla ya 2027 AFCON haijaanza.
 
Miradi mingi ya Majenzi iliyofanywa na Mifuko ya hifadhi haina tija.Kwa sehemu kubwa ni Njia ya wasimamizi wa Mifuko na wanasiasa Kupiga hela kwenye kandarasi za ujenzi.Angalia Majengo mengi kwenye Majiji kama Dar,Arusha na Mwanza yako tupu,hakuna Wapangaji.Fedha za wacahangiaji zinatumika vibaya.Laiti kama tungekuwa na private managers wa pension funds Nchi ingekuwa mbali.Hizi boards za Usimamizi tija zao ndogo.Angàlia like Jengo la NSSF Mwanza pale Kapri Point Hadi Linaanza kuota kitu,hawakufanya feasibility study kama Hotel ya Nyota 5 ni Uwekezaji sahihi Kwa sasa kwa Mwanza.Wameshindwa kupata Kampuni ya Kuendesha hoteli.Kama Serikali Dodoma inajenga Ofisi zake Mtumba,unategemea Nani atakuwa Mpangaji?Kama Serikali ina Sera Mkutano Yake ifanyike kumbi za umma Nani anakuja kuwa Mteja wa conferences?
 
Back
Top Bottom