abdumadutz
New Member
- Jan 31, 2017
- 4
- 3
Dhutous!- injustice (absence of Justice), or violation of right or of rights of another; unfairness; unjust act.
Wapendwa, nilikuwa mwajiriwa katika moja ya kampuni za ujenzi hapa Dar es salaam. Ajira yangu ilikoma mwezi wa tisa 2020. Muda wote nikiwa kazini akaunti yangu ya NSSF haikuwa na fedha. Hapo nyuma zilifanyika juhudi kadhaa zikiihusisha NSSF ili mwajiri apeleke michango yetu NSSF.
Katika nyakati tofauti - 06.10.2020, 13.10.2020 na 07.12.2020 - nilimwandikia Mkurugenzi Mkuu NSSF barua tatu kwamba hakuna fedha yoyote katika akaunti yangu, lakini sikujibiwa!
14.12.2020 nilimwandikia Waziri wa Kazi barua kuhusu hilo; siku nne baada ya barua hiyo, NSSF ikaniita ofisi zake eneo la posta, Dar es salaam na kunambia wanalishughulikia. Hapa nafupisha maelezo, kabla ya hapo niliishafatilia na kufungua madai 24.11.2020, ilishindikana!
06.01.2021 saa tano na dakika kadhaa asubuhi, nilipigiwa simu kutoka NSSF Mkoa wa Mwanza kwamba mwajiri wangu aliweka fedha yangu katika akaunti nyingine aliyonifungulia yeye na sio kwenye akaunti yangu ninayoitumia, na kwamba waihamisha fedha hiyo kuja kwenye akaunti yangu na baada ya wiki mbili watanijulisha. Hakuna kilichoendelea.
06.01.2021 asubuhi kabla ya kupigiwa simu kutoka NSSF Mwanza, niliandika barua nyingine kwa Waziri wa Kazi kwamba hakuna kinachoendelea ndipo nikapigiwa simu! Na nakala za barua nilikuwa napeleka NSSF.
22.01.2021 NSSF Customer Care ikanambia nivumilie suala langu linafuatiliwa, na hapo ni baada ya mawasiliano yangu na Katibu ofisi ya Waziri wa Kazi. Kwa hiyo, mpaka sasa tangu 22.01.2021 hakuna kinachoendelea!
Kwa hakika huu ni udhalili na mateso dhidi ya watu wa hali ya chini; watu wa hadhi ya juu hawaguswi na madhila haya. Watu tunaogopa kusema ukweli.
Jamii yoyote ambamo dhulma kama hizi ndiyo maisha ya kawaida, chuki, uhasama nk. hustawi; ni chukizo mbele ya Mungu Mtukufu, ninavyoamini, wana wa Adamu kuombeana na kutakiana mabaya. MTU unajiuliza ni lini Nusra ya Mwenyezi Mungu itafika katika dhulma kama hizi.
Wapendwa Watanzania wenzangu, naomba mnishauri nini cha kufanya.
Que la paix soit avec vous tous!