Kuna urasimu mkubwa sana kwenye ofisi za NSSF Mwanza ukilinganisha na mikoa mingine, bila kuwa na ndugu au jamaa anayekujua faili lako la mafao linaweza kuzungushwa hata mwaka mzima.
Mimi na wafanyakazi wezangu tuliacha kazi siku moja kwenye kampuni binafsi mimi nikiwa branch ya Mwanza wenzangu wakiwa branch ya Dar. Tulipoacha kazi tulifuata taratibu zote na tukalipwa mkupuo wa kwanza, shida ni kupata mkupuo wa mwisho.
Wenzetu waliofungulia madai yao Dar tayari walilipwa tangu mwezi wa Nne mwaka huu, tuliofungulia Mwanza imekuwa ni danadana tu, ukifika ofisini visingizio ni vingi, utaambiwa malipo yapo tayari lkn bosi wa kuidhinisha kasafiri mara utaambiwa tayari kaidhinisha lkn mje ofisini kuangalia baada ya mwezi, ukienda unaambiwa nendeni baada ya wiki mbili angalieni kwenye akauti zenu, tarehe ikifika unaambiwa nendeni tutawapigia simu.
Sasa ni zaidi ya miezi 6 tunazungushwa huku wenzetu wa Dar tayari wameshasahau kama walikuwa wanadai.
Tunajuta kufungulia madai kituo cha Mwanza, hivi kuna uwezekano wa kuhamisha faili kutoka Mwanza kwenda Dar, au tutakuwa tunapoteza muda zaidi.
Kwa wazoefu wa NSSF tunaomba ushauri.