Asha,
Mimi sio mwanasheria na wala sijitii kujua sheria, ila kwa ueleo wangu kama layman, anachopinga Mbowe mahakamani ni tofauti na mnachosema.
Kwa kusoma maelezo yake ni kama anajaribu kuvuta muda tu ili amri za mahakama zisitekelezwe.
Kuhusu SWAP, alichofanya Mbowe ni tofauti. Yeye alienda bank zingine na kupata mkopo wa kumalizia majengo yake, huku deni la NSSF likiwa bado liko pale pale. Yeye alichotakiwa ilikuwa ni kuiambia hiyo bank nyingine kwamba
ana deni na NSSF lakini halina maslahi, badala yake anataka hilo deni alihamishie kwao na kupata pesa ya ziada ya kumalizia hoteli yake. Hiyo bank nyingine wangempa pesa yote ya kuwalipa NSSF na pesa ya ziada ya kumalizia jengo lake. Angebakiwa na deni la hiyo bank nyingine tu.
Lakini yeye aliamua kuchukua loan ya pili na akawa analipa loans zote mbili, hapo akawa analiwa interest kubwa ya NSSF bila sababu ya maana.
Mi siyajui hayo ya SWAP wala ya SWAT ili uhamishaji wa madeni wataka ushauri wa pande mbili ati. Katika hili NPF chini ya Mkulo inasemekana baada ya kunyimwa cha juu wakaweka kauzibe. Sakata zima laelekea kuwa 'mkomoeni'.
Ya kesi yako bayana,tatizo lako wewe ni kuwa hujazisoma hukumu zenyewe wala hati ya mashatka.
Alichoenda kuuliza Mbowe mahakamani ni je, alipe bei gani? Kwa kuwa kuna hukumu mbili, ya 1999 na ya 2001.
Labda nikuulize wewe mtaalamu wa mafedha? Mbowe alipe bei gani wakati NSSF wenyewe hawajui anadaiwa bei gani?
Na kwanini hawaikamati mali iliyowekwa dhamana na kuipiga mnada badala yake wanatafuta kumkata Mbowe mwenyewe?
Hapa kuna siasa zaidi ya biashara.
Nungwi,
2005 wakati wa kampeni Rostam kwa kushirikiana na Salva, kwa baraka za Kikwete mwenyewe waliitoa hili sakata kwa wahariri wote baada ya NSSF kuwapatia nyaraka zote. Wahariri wakaweka kauzibe, ikaandikwa na gazeti la Mzalendo pekee
Leo linaibuka tena baada ya MBowe kumsema Kikwete na mafisadi wa EPA.
Rostam kazi kwako, umegundua Balile anakupotosha? Ona sasa amekuchonanganisha na Mengi.
Na wiki ijayo akiandika lile suala lingine alilokushauri mlitoe kuhusu mke wa upanga wa Kikwete hakika mtagombana na mkuu wa nyumba.
Na hiyo ndio itakuwa mwisho wako.
Waweke kitomoto Balille na Muhingo kwanza wakupe ushahidi kabla ya kuandika. Wanakuingiza mkenge.
Asha