Nssf tawi la moshi acheni uhuni na utapeli kwa wanachama, mnakera sana

Nssf tawi la moshi acheni uhuni na utapeli kwa wanachama, mnakera sana

gize

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
202
Reaction score
134
Wadau Heshima kwenu

Mtaniwia radhi kama nitakuwa nimekosea jukwaa

Kwa kuwa hapa ni JF basi tuko huru kuongea ukweli bila kumuonea mtu haya kwa lengo la kujenga ili Tanzania yetu isonge mbele.

Nimesikitishwa sana na Huduma Mbovu zinazotolewa na Shirika hili kongwe la hifadhi za jamii NSSF-Hasa tawi la MOSHI.. Nitazungumzia tawi la Moshi kwa kuwa ndipo nilipokuwa nimejisajiri kama member.

Mnamo tarehe 10 October 2013 Niliamua kuacha kazi katika shirika moja hapo Moshi, nikaona heri nikajiajiri tu, sasa kwa kuwa nilikuwa member wa NSSF nikaona heri nikamilishe taratibu zote za kisheria ili nipewe changu nikaanze maisha mbele ya safari

Nilifanikiwa kukamilisha ujazaji wafomu, na utoaji wa nakala zote muhimu walizohitaji.. Hatimaye nikawaomba kuwa kwa kuwa ninaondoka rasmi moshi .. basi naomba pesa yangu itakapokuwa tayari basi niingiziwe katika account yangu.. Muhudumu wa hapo NSSF ni mzee mmoja wa makamu mweusi na mtaratibu hivi (Jina Simjui) Akanimbia basi andika barua ya kuomba hilo suala lako, kisha toa nakala za atm yako ya bank, na kitambulisho cha kura,,, nilikamilisha kila kitu nami nikapewa nakara zangu

Kwa mujibu wa huyo mzee wa NSSF akaniambia tarehe 5 december 2013 Wataingiza hizo fedha katika akaunti yangu
WADAU HADI SASA NINAVYOONGEA HAKUNA HATA SENTI ILIYOWEKWA KATIKA ACCOUNT YANGU

Nikiwa Morogoro tarehe 17 december 2013 , Ilinibidi kufika ofisi ya NSSF tawi la Morogoro.. baada ya kuwaeleza shida yangu.. Basi wakaniambia nisubiri.. na hatimaye wakaniunganisha na watu wa MOSHI, Baada ya Mazungumzo wakaniambia nisubiri WIKI Moja hadi siku 10 check Ipo tayari Mtu wa kuisaini ndiye hayupo atarudi tarehe 27 december 2013.. LEO NI TAREHE 14 JANUARY 2014, HAKUNA KITU. Kwa bahati mbaya sina mtu ninayemjua hapo NSSF Moshi, lakini katika ku google nilifanikiwa kupata simu za NSSF MOSHI ZA MEZANI, Kwa kweli inasikitisha laini zote mbili kila ukipiga zinaita kama mara mbili hivi kisha hukatwa.. na Hadi leo hakuna kilichofanyikiwa.


INasikitisha sana watanzania tupoamua kukomoana wenyewe, na Ki uharisia hili shirika lipo kwa sababu za kodi za watanzania.. na kwa bahati mbaya zaidi inasemekana hata hizo pesa wanazokaa nazo kama michango ya wanachama siku ya kupewa hakuna riba wala gawiwo lolote unalopewa kama faida na huku shirika limewekeza sehemu mbalimbali.

KWA KWELI IMENISIKITISHA SANA, NA NAJUTA KUWA MEMBER WA SHIRIKA HILI.

KAMA KUNA MTU ANAJUA MAWASILIANO YA MTU WA NSSF HASA BOSI WAO NAOMBA ANISAIDIE WADAU.. KWA KWELI INAUMIZA KUONA MTU NI PESA YAKO HALAFU UNAZUNGUSHWA HIVYO.

INASIKITISHA
 
mhhh, pole mkuu.
Nssf ni majanga mkuu, pole, polesana...mimi kuna jamaa yangu ilibidi ahonge laki 2, ili apate milioni 2 zake,, yaani hapo ni full usumbufu na rushwa.. Huduma mbovu.. Mbovu sana... Pole sana, mungu atakusaidia utapata
.
 
Back
Top Bottom