Hiyo ndo ajabu yenyewe! SI hivyo, NSSF wanawaibia sana wanachama wao, pamoja na uwekezaji huo feki (ulaji) utashangaa kuona faida wanayotoa kwa mtu mwenye michango ya milioni nane ni elfu 9 kwa mwaka.
Baba yangu ameamua kususia mafao ya NSSF baada ya kukuta akiba zake wakati anastaafu hazifiki hata laki 5 kwa miaka karibu 35 alofanya kazi (1966-2000)! Wakati anaanza kazi makato ya shs tano yalikuwa makubwa sana, leo NSSF wanamuhesabia shilingi tano ya 1966 kuwa sawa na shilingi tano ya mwaka 2000! Wizi mtupu!
NSSF wangeiga mfano wa PPF kwa kuwekeza kwenye nyumba za gharama nafuu ambazo wanawauzia wanachama wao kwa mkopo; huo ndo uwekezaji wenye akili wenye kumnufaisha mteja badala ya kujinufaisha wenyewe.