Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 73,773
- 102,126
Kwanini mtu anayeacha kazi kwa hiari na alikuwa mwanachama halali wa Nssf hawezi kupewa hela zake mpaka afikishe miaka 55 Yaan umri wa kustaafu?
Mbona kama hii sheria inafavor zaidi upande wa NSSF na sio mwanachama. Kwanini mtu anayefukuzwa au kuachishwa kazi na muajiri ndiyo anapaswa kupewa?
Kwahiyo tuseme kuwa mtu hana haki ya kuacha kazi na akastahili kupewa fedha yake akaendelea na maisha mengine?
Inakuwaje hela mlizokata kwneye mshahara wangu mnipangie namna ya kuzichukua? Kwann nisichukue wakati wowote?
NSSF wabadili sheria yao ya kutoa mafao
Moderator badilisheni title ya uzi, ina mislead...