NSSF wabadili sheria yao ya kutoa mafao


NSSF wabadili sheria yao ya kutoa mafao

Moderator badilisheni title ya uzi, ina mislead...
 
huu uonevu kabisa bila shaka lolote hilo.
wewe nipe hela yngu nikafie mbele. mambo ya kupangiana matumizi watu wazima ni ujinga.
 
Totally true indeed
 
Wanasubiri watetetewe na wabunge. Mliyalea wenyewe sasa ndio nyeusi imekuwa nyekundu mnalia nn
 
Haya ndio mambo ya kuihoji Serikali irekebishe sheria zisizo na maana
 
Mfumo wa mafao ya uzeeni ya Tanzania ni mbovu ajabu.

Tunatakiwa tuwe na mifumo miwili. Mmoja unatakiwa uwe Kitaifa kwa Mtanzania yeyote yule, hii haijalishi alikatwa NSSF au hajakatwa. Ni lazima awe na haki ya kupata mshahara wa kila mwezi anapomaliza miaka rasmi ya kustaafu, mpaka kufa kwake. Tena ziwe ni pesa na mahitaji mengine yote. Hata kama bado anafanya kazi kwengine na muda wa kustaafu umefika, hizi nazo ni lazima alipwe.

Aina ya pili ni hizo za wanaokatwa NSSF au PSSf au utaratibu mwengine wowote, ziwe ni akiba ya mfanya kazi au yeyote aliyekuwa anakatwa au analipa na kuweka kama akiba yake. tena iwe inazaa riba kila mwaka, na anapojitowa tu, wakati wowote kabla hajafa alipwe zote kwa mkupuo na faida yake. Hakuna longo longo.

Hii mifuko haiingiliani, mmoja ule ni wa kitaifa na unatokana na kodi zake, alizokuwa anakatwa moja kwa moja (direct)na anazokatwa "indirect".

Sifahamu kwanini mambo madogo kama haya, yanawaumiza 'wasomi" wetu vichwa. Hayana complications" zozote.

Haihitajiki "rocket science" wala "kikotoo" ushuzi kuyajuwa.
 
Ni wizi tu
Tena ni wizi wa kijinga kabisa.

Mimi nashangaa "complications" zote wanazoziunda za nini? Vitu vyepesi na kwa teknolojia ya sasa hivi, watu hawazidi 50 wataendesha mifumo yote hiyo miwili, niliyoielezea juu hapo. Bila shida yoyote ile. Wala hatuhitaji kuwa na mfumo unaoendeshwa kiserikali. Wawacheieni watu binafsi waendeshe, serikali iwe "facilitator" tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…