NSSF walikataa kunipa mafao yangu hadi niwapelekee cheti Cha kuzaliwa.

Tanki

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
538
Reaction score
246
Hiyo ilitokana na utofauti wa tarehe ya kuzaliwa iliyopo kwenye nyaraka zangu za NSSF na nyaraka zangu uraia.

Utofauti huo ulikuwa ni tarehe tu ila mwezi na mwaka vilikuwa sawa.
Ok, nilifungua madai ya kulipwa mafao yangu. Nikakamilisha Kila kitu.

Nikapewa na tarehe ya kuingiziwa hayo mafao ambayo ilikuwa ni kama mwezi mmoja na siku chache hivi, ila nikaambiwa inaweza hela ikaingia ndani ya wiki mbili zijazo. Naam, wiki mbili mbele nilivyoona kimya nikapiga simu kuulizia, nikaambiwa aisee ilibidi ulipwe tangu wiki iliyopita tatizo lililokwamisha ni utofauti wa tarehe ya kuzaliwa.

Soma Pia: Msaada: Inachukua muda gani kulipwa NSSF tangu kufungua madai?

Nikawaambia nilete kiapo cha Mahakama wakakataa, wakataka Cheti cha kuzaliwa. Ikabidi nianze mchakato wa kutengeneza cheti, ndani ya wiki nikakipata nikapeleka. Wakaniambia watatumia kile cheti kubadili tarehe iliyopo kwenye nyaraka zangu za NSSF baada ya hapo ndipo faili liende Kwa watu wanaohusika na malipo.

Wamesema ni ndani wiki mbili tena zijazo ndo hela inaweza kuingia. Naomba kujuzwa wakuu, Kwa hatua hii iliyofikia Kwa uzoefu wako je itafika wiki mbili kweli?. Maana sitamani ifike hiyo wiki ya pili, na ikifika au ikapitiliza aisee nahisi mtaniokota, maana kwenye hiyo wiki nitakuwa na mambo lukuki ikiwemo na wife natarajia atajifungua wiki hiyo, Kodi ya nyumba wiki hiyo, aisee MUNGU awaguse NSSF waniingizie hizi hela chache kabla ya wiki hiyo ya pili. Yaani angalau isifike tarehe 17. Tuombeane wapendwa
 
Pole sana
NSSF ni wasumbufu sana.
Wanapokata hela hawasumbui ila kulipa ni mizungusho
 
Aina gani ya mafao !
 
Back
Top Bottom