Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umekusanya Tsh. 150.04 bilioni kutokana na tozo za matumizi ya Daraja la Nyerere Kigamboni katika kipindi cha miaka 10 tangu lilipoanza kutumika Mei 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba amesema hayo Jumatatu, Septemba 21, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi kati ya menejimenti ya mfuko huo, wahariri na waandishi wa habari chini ya uratibu wa ofisi ya Msajili wa Hazina.
Soma: Deni la Daraja la Kigamboni (Mwalimu Nyerere) litaisha lini?
Amesema mradi huo katika ujenzi uligharimu Tsh. 345.20 bilioni, zikiwemo Tsh. 328.74 bilioni za ujenzi na Tsh. 16.46 bilioni zilizotumika kulipa fidia kwa wananchi waliohamishwa kupisha ujenzi wa mradi huo.
“Mradi huo ulipangwa kurejesha fedha zilizowekezwa ndani ya kipindi cha miaka 30 na Juni 2026, NSSF ilikuwa imekusanya Tsh. 150.04 bilioni kutokana na tozo za matumizi ya daraja,” amesema.
Pia soma: Serikali yaomba muda zaidi kujibu kesi ya tozo Daraja la Nyerere (Kigamboni)
Katika kipindi hicho, amesema NSSF pia imetumia Tsh. 25.81 bilioni kwa gharama za uendeshaji na matengenezo ya daraja hilo huku mapato yaliyokusanywa yakiendelea kuchangia katika kurejesha fedha zilizowekezwa kwenye mradi.
Chanzo: Mwananchi