Mambo hayafanyiki kwa kusema NITAFANYA.NIKIWA RAIS WA TANZANIA NTAIFANYA TANZANIA KUWA SAFI NA YENYE USTAARABU MKUBWA
Ukweli ni kwamba watanzania sio wastaarabu na wasafi kwa asilimia kubwa sana, wanatakiwa kufundishwa ustaarabu;-
Kila chombo cha habari au social media account wanatakiwa watenge dakika kumi mpaka kumi na tano kila baada ya masaa 6 kutoa elimu ya usafi na ustaarabu kwa wananchi-ni matumaini yangu baada ya mda watu watakuwa wastaarabu na jamii yetu itakua safi tofauti na ilivyo sahivi
Kwenye shule za msingi ndo msisitizo utakuwa mkubwa sana
Mambo ambayo wananchi watahimizwa kila mara
- Hutakiwi kutupa chupa ya maji, au juice hovyo baada ya kutuma
- Hutakiwi kutupa chupa ya maji au juice nje ya gari baada ya kumaliza matumizi yako ni bora utupe ndani ya gari
- Watu watafundishwa namna ya kuosha na kusugua choo
- Watafundishwa namna ya kutumia choo na kuiacha katika usafi
- Watu watafundishwa namna ya kuoga na kujisugua sehemu mbalimbali za mwili
- Watu watafundishwa namna ya kufua nguo mbalimbali
- Watafundishwa namna ya kuosha vyombo
- Watu watafundishwa namna ya kufanya usafi ndani ya nyumba zao
- Watu watafundishwa namna ya kufanya usafi ndani ya ofisi zao
- Watu watafundishwa namna ya kufagia kwenye mazingira ya nje
- Watafundishwa wasitupe taka hovyo na madhara ya kutupa takataka hovyo
IKIWEZEKANA NGUVU ITATUMIKA ILI MAZINGIRA YAWE MASAFI
Elimu itaendana na serikali kuwekeza kwa kuwekaza kwenye maeneo yafuatayo;-
Baada ya mda watu watakuwa wastaarabu na nchi itakuwa safi
- Kuweka dustbin nyingi sana maeneo tofauti tofauti
- Kujenga public toilet nyingi na lengo ni kuwa bure ili kuondoa tabia ya kukojoa hovyo kwenye makopo, kwenye kuta n.k
- Kuharakisha zoezi la kukusanya takataka
Nataka
Itakuwa
Mikakati ZERO.
Hata ukitaka kwenda Kenya, lazima ujue njia ya kupita.