Ntibabanzokiza alikuwa bado mchezaji muhimu sana kwa Yanga

kambale mnene

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2022
Posts
271
Reaction score
197
Nalifahamu sana soka la Tanzania, nazifahamu sana club za Yanga na simba.

Toka nimeanza kuishabikia Yanga ni zaidi ya miaka 40sasa.
Timu zetu hizi mbili Mara nyingi zinakosea kwa kuwaacha wachezaji nguzo ndani ya timu baada zina struggle kufanya vizuri kwenye msimu.

Yanga ilipomuuza msuva mpk leo inastruggle kumpata winga kama msuva au zaidi yake

Simba,ilimuu James kotei,hawajapata mtu kama yule mpk leo.
Haikutosha wakamuuza Luice MIQUISON na chama,simba sasa inatafuta wachawi.

Yanga kumuuacha Ntibazokiza ni kosa kubwa sana.
Yule ni mchezaji Mimi namwita mchezaji baba uwanjani.
Atafuta mipira,anatengeneza nafasi anafunga.
Anakasi,ana nguvu ana kila kitu.

ANAPOKUWEPO UWANJANI KILA MCHEZAJI ANAIGA KUJITUMA KWAKE.

TUTAJILAUMU HUKO MBELE
 
yaani unamwacha Saido alafu unamsajili morison, kwa kweli nyie mnao jiita viongozi mnatakiwa kupimwa akili…..
 
Kama hana nidhamu uendelee kulea tu upuuzi ndani ya kikosi

Morrison uwanjani ni mzuri mbona kaachwa na simba

Kina Balotel waliachwa sababu ya nidhamu mbovu

Hajitambui, umri wenyewe umeenda bado analeta dharau za kipuuzi
Ndo anaenda kumalizia mpira wake huko Singida Big nin sijui
 
Kuna kitu hujaona, Sureboy kiwango kimerudi na combination yake na Aucho imeanza kulipa hawaingiliani sana uwanjani na BM33 anakuja, Mauya yuko fit, Bangala yuko sawa, Yacouba anarudi, Yanga Inatest Double Striker ya Mayele na Makambo na Feisal anapiga namba 10 ya Saidoo na anapasua watu vile vile hii inamaanisha Saidoo japo ni mchezaji mzuri pengo lake halipo ndo maana hakucheza derby na tuliwapasua Mikia aka Makolo FC.

Shida ya Saidoo kuna wakati anajisahau anacheza kama yuko peke yake uwanjan akisaka goli kwa nguvu na kutowapasia wenzake walio katika nafasi nzuri za kufunga! Siku hizi utaalam wa kupiga faulo umeshuka na hawachii wenzake kupiga mwanzo mwisho na ameshakuwa kocha mchezaji badala ya penati kupiga Djuma Shaban yeye anachukua madaraka na kumpa mpira Mayele apige penati ambayo ilipaa na kwenda kutua Uwanja wa Amaan Zenjibari!
 
Makambo aliniuzi sana, Nabi alikuja na mpango kabambe lakini alichokifanya Makambo ni kuuangusha mpango kabambe wa Nabi. Kulikuwa na magoli zaidi ya mawili lakini ana mbwela mbwela tu uwanjani. Hastaili kubakia Yanga huyu Makambo

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
 
Saido ni mchezaji mzuri lkn ana mechi zake. Sio mchezaji wa kutegemewa kuamua mechi. Hana kasi kivile ila ni mzuri kwenye counter attack aki supply mipira kwa haraka sana.

Kosa lake ni dharau na nidhamu mbovu. Alikua amejipatia ufalme jangwani.
 
Makambo sijui anadaiwa huko kwao alikotoka. Maana nafasi ya wazi hata mchezaji wa chandimu anafunga yy anakosa.

All in all Yanga tupate striker mmoja mkali sana wapambanke naamba na mayele, kwenye double striker tuue mapema.

Tunahitaji no 11, 10, 7, 3 na 4 wakali.
 
yaani unamwacha Saido alafu unamsajili morison, kwa kweli nyie mnao jiita viongozi mnatakiwa kupimwa akili…..
Unamwacha mchezaji kwa utovu wa nidhamu, unasajili mchezaji aliyeachwa kwa utovu wa nidhamu
 
Sawa ana tatizo la nidhamu.
Je huyo anayekuja si ndo jambazi kabisa?
 
Ni kweli lakini sifa zote hizo hupotea kwa kukosa nidhamu
 
Basi hujamfuatilia vema huyo Saido, gari linazima muda wowote. Kwenye mechi tsno za mwisho Saido alikuwa akipoteza mipira hovyo. Ni mbinafsi ajabu halafu analazimisha kudrive na kupuga chenga asizoziweza. Alikuwa kero uwanjani kuliko msaada. Wanaodhani Yanga itajutia basi wajifunze soka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…