Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Emmanuel Ntobi, kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ametoa pongezi kwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho, Tundu Lissu, kutokana na ushindi wake wa nafasi ya uenyekiti wa taifa.
Kupitia chapisho lake katika mtandao wa X, Ntobi pia amemshukuru Freeman Mbowe, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, kwa mchango wake mkubwa katika kukuza demokrasia ndani ya chama na taifa kwa ujumla.
Hata hivyo, kauli ya Ntobi imeibua mjadala miongoni mwa wanachama wa CHADEMA na wachambuzi wa siasa kutokana na historia yake ya kumkosoa vikali Tundu Lissu, hususan katika kipindi cha kampeni za uchaguzi wa ndani ya chama.
Ntobi, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga, alijipatia umaarufu kwa matamshi yake ya moja kwa moja dhidi ya Lissu. Katika kipindi cha siku kadhaa kabla ya uchaguzi wa uongozi wa CHADEMA, Ntobi amewahi kumkosoa Lissu kwa kile alichokielezea kama "uropokaji" na kushindwa kuwa na busara katika maamuzi ya kisiasa.
Moja ya kauli zake zilizonukuliwa zaidi ni pale alipomtaja Lissu kama "mropokaji", ‘mbea’ na kumshutumu kuwa hana uwezo wa kutunza siri za chama. Aidha, Ntobi alidai kuwa Lissu hakuwa mtu sahihi kuongoza CHADEMA kutokana na tabia zake, ambazo alizitaja kuwa za kuharibu mahusiano ya chama na wadau wake wa kitaifa na kimataifa.
Pia amewahi kumtuhumu Lissu kufadhili na kuunda kikosi kilichokuwa kinatumia jina la " Sauti ya Wananchi" akishirikiana na watu maarufu mtandaoni na maafisa wa CCM, idara ya usalama wa taifa na Diaspora kwaajili ya kumfitini Mbowe
Aidha Ntobi amekuwa akimuhusisha na baadhi ya matendo yasiyofaa kimaadili kupitia maandikio yake akimuhusisha na "Mzungu" hasa pale Lissu anapokuwa safarini nje ya nchi kama "