Pre GE2025 Ntobi avuliwa Uenyekiti Mkoa wa Shinyanga kutokana na utovu wa maadili na nidhamu dhidi ya Lissu

Pre GE2025 Ntobi avuliwa Uenyekiti Mkoa wa Shinyanga kutokana na utovu wa maadili na nidhamu dhidi ya Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
ni hatu nzuri na muhimu mno, kwa taasisi imara kusimamia nidhamu kwa viongozi waaandamizi wake,

Na bilashaka anaefuata ni Tundu Antipas Mughwai Lisu kuchukuliwa hatua sawa na hizo, maana aina ya uropokaji na tuhuma alizonazo zinafanana kila kitu na huyo muungwana,

ili iwe fundisho kwa wasaliti na waropokaji wengine kama hao 🐒
Mzee wa hovyo nini unatumia kinakufanyqa uwe chizi? Tuonyeshe tuhuma mbili tu za Lissu zinazofanana na Ntobi, usipoonyesha jua tutakuchukulia kama mlevi
 
utamsikiaje na hutaki kuskia?

kwahiyo kibaraka anaenda behind the scenes sio live right?

kwamba kibaraka kuwaita wengine wala rushwa, au wengine wametumwa kugombea umakamu wenyekit kumkabili yeye n.k, huo sio uropokaji gentleman?🐒
Punguza bangi basi, mla rushwa ukimuita mla rushwa ni tusi? Ndio maana CCM usipokuwa mla rushwa hupati uongozi, hamtaki kusikia anayekemea wala rushwa.

Kusema kweli haijawahi kuwa uropokaji kwa wenye akili timamu labda vilaza
 
Kamati tendaji ya Kanda ya Serengeti katika kikao chake cha jana Jumatano Januari 08, 2025 kimefikia maamuzi ya kumvua Uongozi Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Bw. Emmanuel Ntobi kutokana na utovu wa nidhamu na maadili ikiwemo kuchafua Viongozi wa Chama chake Kitaifa kupitia mitandao ya Kijamii.

Akizungumza ma JamboTv Usiku huu (Januari 09, 2025) Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la CHADEMA Kanda ya Serengeti Lucas Ngoto ameiambia JamboTv kuwa maamuzi hayo ya Kikao yamefikiwa Kisheria ikiwa ni mara baada ya kumpa fursa ya kuweza kujitetea dhidi ya kauli na maandiko yake kadhaa yasiyokuwa na utu na heshima kwa Viongozi wa Chama Taifa.

Ntobi ambaye pia mwaka 2023 aliwahi kusimamishwa Uenyekiti wake kwa mwaka mmoja kutokana na makosa ya kinidhamu, amejitanabaisha mitandaoni kama muungaji mkono na Mpiga kampeni kwaajili ya Mhe. Freeman Mbowe kuweza kurejea tena madarakani kama Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, amekuwa na mfululizo wa maandiko kadhaa, yenye nia ya kumchafua, kumtweza na kumtusi Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe. Tundu Lissu ambaye pia ni Mshindani na mgombea mwenza wa Mhe. Mbowe kwenye nafasi ya Uenyekiti wa Chadema taifa kwenye uchaguzi utakaofanyika baadae mwezi huu.

Miongoni mwa kauli zake ni pamoja na kumuita Makamu mwenyekiti huyo kuwa Mropokaji, Mmbea, sambamba na kumtuhumu kufadhili na kuunda kikosi kilichokuwa kinatumia jina la "Sauti ya Wananchi" akishirikiana na watu maarufu mtandaoni na maafisa wa CCM, idara ya usalama wa taifa na Diaspora kwaajili ya kumfitini Mhe. Mbowe

Aidha Ntobi amekuwa akimuhusisha na baadhi ya matendo yasiyofaa kimaadili kupitia maandikio yake akimuhusisha na "Mzungu" hasa pale Mhe. Lissu anapokuwa safarini nje ya nchi kama " Soon ataweka wazi faragha za Mzungu wake" pamoja na "Si tuliwaambia jamaa yenu kakimbilia kwa mtasha wake? kiko wapi?", mwisho wa kunukuu.

============== ==============

JOHN MNYIKA AULIZWA
JamiiForums ilipowasiliana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika akasema “Naomba wasiliana na Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti au Katibu wake kwa kuwa maamuzi hayo ni ya Kanda ya Serengeti na wao ndio watakaosema kama ni taarifa sahihi au sio sahihi.”

UONGOZI WA KANDA WANENA
JamiiForums imewasiliana na Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti (CHADEMA), Lucas Ngoto amesema:

“Ni taarifa ya kweli, kikao kilifanyika Januari 8, 2025, Shinyanga Mjini, alipewa nafasi ya kujitetea, akatakiwa kuondoka kwenye kikao baada ya hapo ili maamuzi yafanyike ndipo taratibu za maamuzi zikaendelea.

“Maamuzi yameshafanyika, Ofisi ya Katibu inaandaa barua ili imjulishe maamuzi ya kikao, bado hajakabidhiwa majibu rasmi licha ya kuwa maamuzi yameshatoka.”

Pia soma
Wasingemvua kipindi hiki cha chaguzi.
Wangesubiria hadi uchaguzi upite.
Vinginevyo itaonekana ni upande wa mpinzani wa Ntobi ndo ume-engineer.
 
kwani humuungawana kusema kwamba huyo kibaraka wa mabenyenye ya magharibi anashiriki ndoa za jinsia moja, kosa lake liko wap gentleman 🐒
Punguza bangi basi, mla rushwa ukimuita mla rushwa ni tusi? Ndio maana CCM usipokuwa mla rushwa hupati uongozi, hamtaki kusikia anayekemea wala rushwa.

Kusema kweli haijawahi kuwa uropokaji kwa wenye akili timamu labda vilaza
 
Mzee wa hovyo nini unatumia kinakufanyqa uwe chizi? Tuonyeshe tuhuma mbili tu za Lissu zinazofanana na Ntobi, usipoonyesha jua tutakuchukulia kama mlevi
Kibaraka ameolewa ughaibuni na ndume mwenzie,
kweli si kweli?🐒
 
Umesahau matusi ya Nape kwa Marehemu Lowasa? Au matusi aliyotukanwa Mzee Salim Ahmed Salim aliposhindana na Kikwete 2005? Au umesahau alivyozabwa kibao Mzee Warioba pale Ubungo 2014 ,na aliyemzaba sasa ni kiongozi mkubwa serikalini?
Huyo alikuwa kwao Nanjilinji huko anakula panya na kunywa Nipa.
 
Inavyoonekana yeyote anayemkataa mkubwa hana nidhamu! Ntobi anampinga Lissu kwa nguvu zake zote na Lissu anampinga Ayatollah Mbowe kwa nguvu zake zote!
Kwa akili finyu iliyopofushwa na matamanio ya moyo. Bahati nzuri ushahidi wa post za Ntobi zimewekwa humu jukwaani, za Lissu zimewekwa kwenye akili na mioyo ya wapuuzi
 
kwani humuungawana kusema kwamba huyo kibaraka wa mabenyenye ya magharibi anashiriki ndoa za jinsia moja, kosa lake liko wap gentleman 🐒
Ndoa za aina moja? Inaelekea alikutaliki ndio maana unamtolea siri
 
Kwa akili finyu iliyopofushwa na matamanio ya moyo. Bahati nzuri ushahidi wa post za Ntobi zimewekwa humu jukwaani, za Lissu zimewekwa kwenye akili na mioyo ya wapuuzi
Umepotoka; usidhani kila mtu hapa ni shabiki wa Mbowe au Lissu. Whoever wins kwangu makes no difference. Ninachokisema mimi ni kwamba huu ni msimu wa uchaguzi; ni vizuri wanachama wakawa huru kuchambua strengths/weaknesses za wagombea ili waweze kuweka madarakani viongozi wanaowaona wao wanafaa!
 
Hii ni lugha tofauti na niliyorespond, simamia post yako. Kupinga anavyopinga Ntobi ni kashfa na kejeli, na ndio maana chama kimemchukulia hatua. Lissu wapi ametoa kashfa na kejeli? Una mapenzi hauko fair usizunguke
 
Back
Top Bottom