Ntotofula Natural Swimming Pool- Mbeya

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Ntotofula Natural Swimming Pool

NTOTOFULA ni neno la Kinyakyusa lenye maana ya Povu, Sehemu hii ya kuogelea inayopatikana ndani ya Mto Mbaka katika kijiji cha Mbambo Halmashauri ya Busokelo iliitwa hivyo kutokana na uwepo wa povu la asili litokanalo na maji kujipiga kwenye Mwamba/mawe ama ukuta wa asili. Eneo hili limekuwa likitumika kutoka kizazi hadi vizazi kwa shughuli za kuogelea kwa wakazi wa maeneo haya.

Uongozi wa Gwankaja Farm lodge wameamua kufanya juhudi mbalimbali za kuongeza thaman eneo hili ikiwemo kulitangaza ili liweze kutumiwa kwa shughuli za kiutalii na michezo ikiwemo kuogelea ama kupunga upepo.

Gwankaja Farm lodge ni sehemu inayopatikana umbali wa kilomita ishirini na saba tu (27) kutoka Tukuyu Mjini ambayo mgeni anaweza kupata huduma mbalimbali kama vile kupiga kambi (Camping), Malazi, Chakula N.K, Hii kuifanya sehemu hii kuwa muhimu sana kutokana na ukaribu wake kwenda kwenye vivutio mbalimbali hasa vile vipatikanavyo Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.

Credit: Mazplusfly | Photobank studio | Uyole cultural tourism enterprise

 
Wapelekeni kibugujo na na mbugujo ( maporomoko ) ya mwalisi river watainjoi sana mkuu.
 
Ko mm mwenyej wa isabula Nairobi nikitaka kuinjoi maisha ntotofula ntalipishwa pesa???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…