Nufaika na Internet, hii ndio sehemu muafaka ya wewe kunufaika

Sitaki kukukatisha tamaa wala sitaki kuonekana napinga jitihada zako za kujiinua kiuchumi.

Ila nauliza tu,
1. nini kinakua dhamana mpaka mtu atume pesa yake kwako kwa ahadi ya kuunganishwa na group la whatsapp?

2. Ni kitu gani unatoa cha ziada sana ambacho hapa jf hakipo, wala youtube hakipo, wala kwenye blogs na tovuti mbalimbali hakipo?

3. Anayelipa atapata uhakika gani kwamba kwenye hilo group lako atajifunza kitu kipya ambacho hakuwahi kukijua?

4.Wasifu wako ukoje, kitaaluma?

5. Endapo mtu akilipia na asiunganishwe je atalalamika wapi? Haki yake itapatikanaje?
 
Una Idea ila kuiweka sokoni inakuwa vigumu? Tengeneza wajinga wengi sana akilini mwako na utatoboa
 
Safi sana, Umeuliza maswali mazuri mno.
Ningependa kukufahamisha tu kwamba Mimi ni kijana Mtanzania ambaye nipo katika harakati za kuwasaidia Watanzania. Kuhusu elimu yangu ni (Bachelor of Science with Education) na ninaendesha Blog ya Nufaika na Internet. Ningeweza kuweka link lakini Jamiiforums hawaruhusu na nimeshawahi kupata BAN. kwa kuweka link.
katika blog yangu ya Nufaika na Internet nimejieleza kwa undani sana na pia nimeweka Links za profile zangu za mitandao ya kijamii, twitter na Facebook.
Hivyo kama unataka kunifahamu kiundani na kujua maarifa ninayotoa yana thamani gani , naomba nitumie ujumbe WhatsApp nikutumie Link.
Ahsante sana na Karibu!
 
Ajibu haraka au na akae kimya milele ili watu wasijegeuzwa mitaji kwa kuwa anafahamu kila mtu ana shida ya kujikwamua kiuchumi!
 
Teh teh teh vyuma vimekaza hadi wanabuni njia mbadala

Kama unafaka elimu ingia youtube au Google, achaneni na udanganyifu
 
Ahsante kwa maoni yako.
Natoa ujuzi kwa ridhaa ya anayetaka kujifunza.
Ni kwetu tu tanzania hatujui haya mambo lakini wenzetu nje wana mitandao( Kama Udemy na Tutorvista) inayotoa huduma za mafunzo mtandaoni na zimewasaidia wengi.
Cha ajabu sisi tunaiga ya kujifurahisha tu huku tukipoteza muda wetu.
Hapa angetokea mtu anauza program za GAME KALI ZA RACING AU NYINGINEZO INGEKUWA RAHISI NA WATU WENGI WANGECHANGAMKIA.
ILA MAARIFA YA KUMJENGA MTU WENGI WANAPUUZA.
Nimejitoa kuwasaidia kwa wanaotaka na wasiokuwa tayari, Waendelee kutafuta elimu Google na YouTube itawasaidia pia.
 
Umejitafutia mradi wa kupata pesa na HUJAJITOA KUWAPA WATU ELIMU. Otherwise malipo yasingekuwepo
 
Yapo mafunzo ya bure na mafunzo ya kulipia.
Juzi niliweka tangazo la mafunzo ya bure ya Graphics Design.
Yameanza tangu juzi na bado yanendelea hadi sasa. Ni bure kabisa mtu halipii hata tsh mia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…