Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Salaam Wakuu,
Thread hii iwe ndo thread kuu itakayosheheni Nukuu za Amri Jeshi na rais wa JMT Samia Suluhu. Usisite kuweke nukuu yake ukikutana nayo.
“Kwa wale ambao wana mashaka Mwanamke huyu ataweza kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, nataka niwaambie aliyesimama hapa ni Rais. Aliyesimama hapa ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye maumbile yake ni Mwanamke” Machi 22, 2021
‘’ Mnaua Wafanyabiashara (kwa kutumia nguvu kukusanya kodi) mnapunguza walipa kodi, nendeni mkatengeneze na kutanua wigo wa walipa kodi, yale mengine yanayowapunguzia Watu ari ya kulipa kodi Waziri (Mwigulu Nchemba) naomba ukayasimamie” Aprili 1, 2021
“Trend mnayokwenda nayo sasa mnaua Wafanyabiashara, mnatumia nguvu zaidi kuliko akili na Maarifa kupata kodi, sasa wale mnaowakamua mkienda mkachukua vifaa vya kazi, mkafungia akaunti zao na kuchukua pesa kwenye akaunti, akitoka anafunga biashara anahamia Nchi ya Pili” Aprili 1, 2021
“Serikali ni moja pasitokee kuvutana, nendeni mkawatumikie Wananchi, mkafanye kazi baada ya Bunge la Katiba,kwa sasa mko kwenye Bunge la Katiba aah! hivi nina maradhi gani na Katiba!?, nadhani kwakuwa wameni-push push sana Katiba, Katiba lakini kwa sasa wasahau kidogo” Aprili 1, 2021
“Nafahamu 2025 ipo karibu na kawaida yetu inapoingia kipindi cha pili cha Rais aliyopo Watu kidogo mnakuwa na lile na hili kuelekea mbele, nataka kuwaambia acheni, twendeni tufanye kazi hili na lile tutajua mbele” Aprili 1, 2021
“Nataka kuwaambia rekodi yako inakufuata katika maisha yako, wengine wamekosa hizi nafasi kwa rekodi zao tu, na Mimi nitakuwa na jicho kubwa sana pamoja na kwamba yamelegea lakini yanaona, nitakuwa na jicho kubwa kuangalia rekodi zenu” Aprili 1, 2021
“Nitakuwa na jicho kubwa sana kuangalia rekodi zenu na safari ya mbele yetu lakini nataka kuwaambia kila yule mwenye nia ya 2025 aache mara moja” Aprili 1, 2021
“Nataka kuwaambia rekodi yako inakufuata katika maisha yako, wengine wamekosa hizi nafasi kwa rekodi zao tu, na Mimi nitakuwa na jicho kubwa sana pamoja na kwamba yamelegea lakini yanaona, nitakuwa na jicho kubwa kuangalia rekodi zenu” Aprili 6, 2021
“Watanzania tunakaribia Milioni 60 na zaidi ya Watanzania Elfu 5 walikuwa na sifa za kukaa mlipokaa leo lakini Mungu akaona nyinyi mpate nafasi, mlioapa leo nendeni mkafanye kazi”. Aprili 6, 2021
“Nataka niseme tukikuta bango moja aidha Mkurugenzi au Mkuu wa Wilaya umekwenda na hii haina maana mkazuie Watu kuandika kero zao, kero za Wananchi mkashughulikie na tukikuta malalamiko kwamba mnawafinya wasiseme hivyohivyo tutawashughulikia”.
"Wewe ni kijana, mimi ni mama, ukinizingua, tutazinguana." Aprili 6, 2021
“Wawekezaji wanataka kuja Tanzania lakini kwa mambo yetu wanakimbia, tuvute tena uwekezaji, tupate ajira,fedha izunguke,uchumi ukue, nikiwa Makamu wa Rais kuna Mwekezaji alikuja, sijui alitishwa nini!, nadhani kaambiwa tutakupiga kosa la uhujumi uchumi, akaondoka”. Aprili 6, 2021
“Nendeni mkawe Wabunifu, sitegemei uzembe wa makusudi, nendeni mkafanye maamuzi, mnachelea sana kufanya maamuzi, kama mlichelea wakati ule sasa niko Mama, nimeshawaambia ukifanya ya hovyo tutazinguana, unataka kufanya umekwama njoo tuzungumze” Aprili 6, 2021.
"Nchi yetu imekuwa ikilalamikiwa kwa kutokuwa na sera nzuri ya uwekezaji ikiwemo urasimu mwingi, utaratibu mbovu wa kodi, na ucheleweshaji wa kutoa vibali na leseni" Aprili 22, 2021 Bungeni/Dodoma