Juzi nikaamua kuhamia Amazon, strange thing happened, kwny bei ukitoa gharama za bidhaa ynyew na shipping fee naona wamecalculate na TAX
Kuna baadhi ya majimbo USA huwa na Tax na Mengine ni Tax free (Viz: Alaska, Delaware, Montana, New Hampshire) hii ni moja.
Pili kuna baadhi ya Bidhaa ukinunua ndani ya USA huwa kuna tozo la kodi, na hii utaiona wakati unafanya malipo
Nnavyojua pale posta mzgo chini ya 2kgs haulipiwi kodi,
Huo wa kwangu ni above that.
Kwa uzoefu kidogo niliokuwa nao iko hivi.
- Waweza kuwa na mzigo chini ya 2Kg, ila unathamani kubwa, iwapo utafuata hatua za ukaguzi stahiki, Lazima ulipie kodi.
- Waweza kuwa na mzigo zaidi ya 2Kg, usilipie kodi, ila ukatakiwa kulipia fedha ya stemp ambayo huwa haizidi TZS 3,500 (Sio mara zote hili kujitokeza)
Sasa swali langu ni je? Mzgo ukifka hapa bongo pale posta hawatanilima tena mambo ya TRA cause nilijuta mzgo wangu wa kwanza kuja nililimwa kodi kubwa adi nikajuta.
Reje maelezo hapo juu.
Kulipa kodi ndani ya USA, si kigezo cha kutokulipa kodi hapa nchini kwa mzigo unaopaswa kulipiwa kodi.
Ni vyema ukajiandaa kwa kulipa kodi
Na ikitokea mzigo ukatoka bila kudaiwa kodi basi itakuwa ni faida kwako.
KARIBU