Nitumie nafasi hii na mimi kutoa mrejesho wangu kuhusu hii huduma.
Mnamo tarehe 8/12/2017 nilifanya maamuzi ya kutumia hii huduma kwa mara ya kwanza kwa kuwa nilikuwa na hitaji simu aina ya XIAOMI MI5x(China) au MiA1 (global).
Niliwasiliana na Mwl. RCT kwa WhatsApp kama alivyo elekeza katika hii thread. Akanitajia gharama siku hiyo nikafanya malipo kwa mpesa kwenda kwenye Account yake aliyo nipatia.
Nilikuwa na mawazo sana hiyo siku mtu simfahamu halafu nimemtumia kiasi kikubwa cha pesa basi nikajipa moyo. Pia baadhi ya member humu walinitia moyo niwe na imani.
Baada ya siku kama saba Mwl. RCT alinipatia tracking number ambayo hutolewa ilikufuatilia mzigo kila hatua, siku kama tatu mbele nilianza kupata update za shipment ya mzigo wangu.
Ilichukua kama week mbili mzigo kufika dar.
Na kwakuwa nilikuwa dar mzigo wangu nilichukua siku ya jumatano ya tarehe 3/01/2018 PPF TOWER POSTA nikajiridhisha mzigo ndiyo wenyewe, then tukakabidhiana.
Mwl. RCT Mungu akubariki sana kwa uaminifu ulio nao, kwa pesa unazotumiwa ungekuwa na tamaa ungeweza kufanya chochote lakini unathamini kile kidogo unacho kipata kupitia hii huduma yako.