kingjohn255
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 400
- 513
Watu wengi wamekuwa na utaratibu wa kununua gari wanazotamani kuwa nazo, lakini ukweli ni kwamba matumizi ya gari kuna muda ni makubwa kuliko uhalisia wenyewe, mimi kama muagizaji na muuzaji wa magari leo napenda kuwashauri jambo moja kuhusu fomula ya kutumia gari. Nunua gari ambayo unaweza kutumia asilimia 30% tu ya mapato yako ya mwezi kwa ajili ya uendeshaji wake kwa mwezi, kwa maana kuanzia mafuta na marekebisho yake madogo(minor services) kama oil, plug, nk, na usipende kununua gari uitakayo kwa sababu unaweza kutamani Premio ila uhalisia uwezo wako ni Passo.