Nunua kitu kwa kuzingatia unahitaji nini hasa kutoka kwenye bidhaa husika

Nunua kitu kwa kuzingatia unahitaji nini hasa kutoka kwenye bidhaa husika

Vhagar

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
20,550
Reaction score
39,949
Kama una pesa za kupoteza yaweza usijali sana.

Wafanya biashara na watoa bidhaa wanafanya kila mbinu kuitaka pesa yako. Wana kila mitego ambayo usipoangalia unaweza kuwa mtumwa wa kununua vitu bila mpango. Matangazo kila station ya redio na tv kupamba bidhaa.

Hii kesi hasa ni kwa bidhaa za elecronics.
Unanunua tv kubwa ya 4k na smart os kwa bei kubwa. Mwisho wa siku huna content yeyote ya 4k unayoitazama kutoka kwenye hiyo tv. Hizo feature za smart ni za kulipia kila mwezi + mabundle bei juu. Toka ununue huna mpango nazo. Kumbe tv ya kawaida na bei stahiki tu ya FHD ingekufaa.

Leo umenunu simu hii kwa million moja baada ya mwaka inatoka aina nyingine kwa millioni mbili. Kisa umesikia kuna vitu flani imeongezewa. Unakuta hata ile kwanza hukuzingatia kwamba features nyingi wala hukua na kazi nazo.
Umeona nguo kisa tu umeipenda unainunua ukizingatia muuzaji amekushawishi. Unavaa mara moja then unaachana nayo inaozea kabatini.

Umepewa ramani na mchoraji ya nyumba umeipenda design tu kijuu juu. inajengwa inawekwa kila makororo mengine huna hata mpango nayo hapo kwako zaidi yamekuongezea gharama zisizo na msingi. Jumba limekuwa kubwa na uko ww tu na mkeo hata hao watoto muda mwingi wako shule.

Ni vyema kukitambua kitu na kuwa na sababu na kitu kabla hujafanya maamuzi kujua je kwanini nakihitaji.Je, kwa mahitaji yangu hiki kitaendana na mimi?

Unaweza nunua kitu cha mamilioni kumbe kwa matumizi yako kifaa cha laki tano tu kingetosha sana.
 
Hela yako unapangiwa jinsi ya kutumia
Hivi unajua kutamani kitu hata kiwe sh ngapi kikubwa uwezo wa hiyo hela unayo

Maisha yenyewe mafupi haya
Ishu wakati mwingine si hata kuwa na pesa ni kutokujua na mkumbo.
 
Kama una pesa za kupoteza yaweza usijali sana.

Wafanya biashara na watoa bidhaa wanafanya kila mbinu kuitaka pesa yako. Wana kila mitego ambayo usipoangalia
Umenena sana watu wengi hufuata mkumbo ili kuonesha ufahari hasa kwenye hizi simu. Mtu ananunua simu ya bei juu lkn matumizi yake ni whatsap tu na Facebook
 
Ujumbe huu usiwe tu kwa wanawake bali watu wote.

Uhuru wa kutumia hela yako jinsi utakavyo hakuna anaweza kuzuia ila ni ushauri tu ambao unaweza kuutekeleza ama ukaachana nao.

Hali za uchumi kama taifa na dunia sio nzuri kiujumla, sio wakati huu tu bali hata siku za nyuma na huko tuendako pia.

Elimu ya matumizi bora na manunuzi bora na yenye tija inatakiwa sana nyakati zetu hizi, kwa maslahi mapana ya taifa na kizazi kijacho , ni lengo lile lile la kupunguza umaskini.
 
Na kitanda pia uchonge futi 2 kwa 6 ,
size 6 by 6 chote cha nn?

Wakati unalala sehemu ndogo?.


Sisi tunamiliki vitu vya gaharama kwa sababu ya maintain status .

Sio kingine.
 
Back
Top Bottom