INAUZWA Nunua mashine za kutotolesha vifaranga zenye ubora kwa bei poa

INAUZWA Nunua mashine za kutotolesha vifaranga zenye ubora kwa bei poa

Urban86

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
279
Reaction score
130
Tunauza mashine mpya za kutotolesha vifaranga.

Mashine zetu ni mpya na zenye ubora wa hali ya juu. Kwa sasa tunauza mashine za kutotolesha mayai 1056 na mayai 528. Inatumia umeme wa 220V na power consumption ni 200W (ya Mayai 1056) na 140W (ya mayai 528)

Sifa za mashine zetu:.

1. Zina mashine ya digitali(micro-computer) kwa ajili ya kudhibiti kiasi cha joto na unyevu.

2. Zina sehemu ya kuweka mayai na kutotoleshea vifaranga kwa pamoja.

3. Zina feni 2 ambazo husamabaza kiasi sawa cha joto na unyevu kwenye mayai

4. Zina mfumo wa kuzungusha mayai ili kupata kiasi sawa cha unyevu na joto.

5. Zinatumia kutotolesha mayai ya kuku, bata, bata mzinga, njiwa na ya ndege wengineo.

6. Zimetengenezwa kwa materials ambayo huweza kuhifadhi joto kwa hadi masaa 5 mara baada ya kukatika kwa umeme.

7. Zina ufanisi wa kutotolesha mayai kwa hadi 95% ya mayai kulingana na ubora wa mayai.

Vifaa vya Ziada

·-------- Pc 1 ya hita ya joto(Temperature heater)

·-------- Pc 1 ya tochi ya Mayai(Egg candel)

·-------- Pc 1 ya hita ya unyevu(Humidity heater)

·-------- Pc 2 za switch( limited switch)

Tunatoa waranti ya mwaka 1 na ushauri wa jinsi ya kutumia mashine hizi ili kuweza kupata ufanisi mkubwa.

Bei zetu ni poa sana. Mashine ya mayai 1056 tunauza 3,300,000/= na ya mayai 528 tunauza 2,300,000/=. Wasiliana nasi kwa namba 0783 095 169 na 0755 571604(Whatsapp) tupo Dar. Tunatoa usafiri bure kwa maeneo ya Dar na kama upo mkoani utalipia kiasi cha gharama za usafiri.
Karibuni sana
 

Attachments

  • 1434206513462.jpg
    1434206513462.jpg
    46.9 KB · Views: 1,338
  • 1434206537659.jpg
    1434206537659.jpg
    43.6 KB · Views: 1,142
  • 1434206811884.jpg
    1434206811884.jpg
    39.5 KB · Views: 1,040
  • 1434206841208.jpg
    1434206841208.jpg
    56.7 KB · Views: 1,013
  • 1434206862138.jpg
    1434206862138.jpg
    49.7 KB · Views: 1,005
  • 1434206889998.jpg
    1434206889998.jpg
    36.3 KB · Views: 1,003
  • 1434206913298.jpg
    1434206913298.jpg
    55.5 KB · Views: 1,020
mi nataka ndogo ya angalau mayai 100 kulingana na pesa yangu kidogo
 
Nakuelewa mkuu Kigger, kwa sasa tunazo za mayai 528 na ya mayai 1056. Baada tutakuwa na size za chini zaidi mkuu
 
umeme wa tanesco ni shida ndg. siku 21 mfululizo bila kukata zaidi ya masaa matano kwa cku kweli? hamna zinazotumia aina nyingine ya power mfano solar?
 
Je kama utawekeza kwenye incubators gharama zako zitarudi na Kupata faida?
Ni swali la kawaida ambalo utajiuliza kwamba, muda gani itachukua kurudisha gharama zako za awali. Hebu soma kwa makini mfano huu:
Hebu tuchukulie umewekeza takribani, (4,000,000sh) kwenye mashine ya mayai 1056. Utakuwa na uwezo wa kuzalisha takribani 352 vifaranga kwa wiki. Gharama zako hasa zitakuwa kwenye mayai yaliyorutubishwa na umeme. Hapo tuchukulie umekupata mayai yaliyorutubishwa kwa (400sh)@ mayai na (50sh) kama umeme utakaotumia kwa YAI, hivyo jumla ya gharama za kuzalisha kifaranga ni wastani (450sh Kifaranga. Kama utauza vifaranga vyako vyenye siku 1 kwa (1000sh) (makadirio ya haraka, inaweza kuwa zaidi), utatengeneza faida ya (550sh) @ kifaranga. Kama ukizidisha (550sh) kwa mayai 352 kwa wiki, utakuwa umetengeneza (193,600sh) kwa wiki. Sasa chukua mtaji wako uliowekeza awali wa (4,000,000sh) ugawanye kwa faida yako ya kila wiki ya (193,600sh), utarejesha gharama zako ulizowekeza awali ndani ya kipindi cha wiki 20 = miezi 5. Kama utabadilisha kidogo hizo namba hapo juu, utakuta muda mrefu kabisa utakaochukua kurejesha gharama zako za awali ulizowekeza itakuwa miezi 6. Hivyo jibu ni kati ya miezi 4 mpaka miezi 6.
Unaweza kutengeneza kipato zaidi ya hapo kwa kufanya biashara ya kutotolesha mayai, na kuzalisha vifaranga kasha kuwalea na kuwauza kama kuku wazima. Kiukweli gharama zako zitarudi mapema zaidi na Kupata faida na faida.
Kwa nini sasa usiwekeze fedha zako kwenye mashine itakayo kuzalishia kipato zaidi kisha kukununulia “your luxuries” kuliko kununua luxuries ambazo zitapunguza kipato chako?
KARIBU TUWEKEZE KWENYE INCOME GENERATING ASSET!
 
Last edited by a moderator:
umeme wa tanesco ni shida ndg. siku 21 mfululizo bila kukata zaidi ya masaa matano kwa cku kweli? hamna zinazotumia aina nyingine ya power mfano solar?
kweli mkuu tanesco hawaaminiki
 
maskini tutaweza hizo bei .sisi wa vijijini umeme shida.tunasolar tu
 
Best way nikuwa na back up ya jenereta mkuu. Zipo incubator za solar ila gharama zake ziko juu zaidi pia hazitotoleshe mayai mengi kama hizi za umeme wa kawaida.
 
Vipi kuhusu gharama za Umeme?
Mashine ya mayai 1056 inatumia umeme wa 220-240V na Power consumption ya 200W na ya mayai 528 inatumia umeme wa 220-240V na 160W power consumption.
Kwa maana hiyo kwa masaa 24 inatumia unit 4.8 i.e. (200x24/1000= 4.8kWh) za umeme na kwa siku 21 za utotoleshwaji wa mayai itatumia umeme wa units: 4.8x21=100.8 ambazo ukizizidisha na bei ya unit moja say 310Tshs. Hivyo kwa mwezi utatumia umeme wa 31,250Tshs.
Nachotaka kuwaonyesha hapa ni kwamba, ukinunua mashine yenye uwezo sawa na huu lakini inatumia umeme say 400W(power sababu voltage itabakia 220-240) utalipia umeme wa 31,250Tshs zaidi, na ukitotolesha mara 15 kwa mwaka (365/21= 17 average) utatumia umeme wa 468,750Tshs kama hasara katika gharama za uendeshaji wa mashine.
 
Incubators: Changamoto zake, Jinsi ya kupata ufanisi mzuri na mafanikio zaidi kwenye incubator yako.


Kulingana na utafiti uliofanywa, matatizo ya uzalishaji wa kuku ambayo wafugaji wa kuku wanakabilina nayo kwa kutumia mashine za kutotolesha vifaranga na huchangiwa na mambo yafuatayo:
1. Wafugaji hawafuati maelekezo ya kutumia incubator (mashine ya kutotolesha vifaranga).
2. Wafugaji hawajaribu (test)kwanza utendaji wa Incubator tupu, ili kupata uzoefu wa kurekebisha joto na unyevu, vitu/hali ambavyo ni muhimu sana kwa ufanyaji kazi sahihi wa Incubator. Kabla ya kuweka mayai yako katika Incubator, unapaswa kuiwasha kwa angalau wiki moja ili kuweza kuelewa jinsi inavyofanya kazi.
3. Wafugaji husahau kujaza maji kweye beseni (basin) la incubator hivyo husababisha mayai kukauka na kutokutotolewa.
4. Wafugaji hushindwa kuchagua mayai bora na yaliyorutubishwa ya kuweka kwenye incubator kwa kuyaangalia (scanning) kwa kutumia tochi ama egg candle.
5. Wafugaji kusahau kugeuzageuza mayai mara kwa mara ikiwa incubator zao hazina mfumo wa automatic wa kugeuza mayai; hii husababisha mayai kukaangwa (frying).
Matokeo ya haya husababisha wafugaji hupata hasara, kuvunjika moyo, kukata tamaa na kuishia kulalamika kuhusu ubora wa incubator.


Kimsingi incubator yeyote mfugaji atakayochagua, mafanikio ya kutotolewa mayai yote, kwanza kunategemea juu ya ubora na urutubishwaji (fertility) wa mayai yanayokwenda kutotoleshwa, na pili, juu ya uangalifu na usimamizi wa Incubator. Jinsi utakavyoindesha vizuri ndivyo utakavyopata mafanikio zaidi. Umewekeza au unapanga kuwekeza fedha zako, basi unapaswa kuwa mweledi (professional) vinginevyo utapoteza fedha zako pamoja na mayai. Ufanisi wa matumizi bora ya Incubator ndogo unapatikana pale ambapo 80% hadi 90% ya mayai yanapofanikiwa kutotoleshwa vizuri.


Hizi ni baadhi ya dondoo tutakazo kuwa tunapeana juu namna ya kupata matokeo bora kwa incubator yako.
Pia tunauza incubator bora na za uhakika kwa bei nafuu. Incubator zetu ni mpya, (full automatic)zinatumia kompyuta ndogo kudhibiti kiasi cha joto na unyevu, zinageuza-geuza mayai zenyewe, zina feni 2 za kusambaza kiasi sawa cha joto na unyevu kwenye mayai. Mashine zetu zinatumia kiasi kidogo cha umeme, pia zinaweza kuhifadhi joto na unyevu kwa hadi ya masaa 5 mara baada ya kukatika umeme hivyo kukupa nafasi ya kuunganisha generator bila mayai yako kuathirika kwa kukatika umeme.Tuwasiliane kwenye 0783 095 169 au 0755 571604 ikiwa utahitaji incubators zetu.


Nawatakia mafanikio kwenye miradi yenu ya ufugaji
 
Tutor B


Best Regards,
Imma Salingwa,
PDPR Director, www.envaya.org/pdpr Phone: +255 7543987178, +255
652556833

Bahatimbaya sijui kuweka link watafute hao, wana bei nzuri sana, pia mizinga na mashine za kutengenezea mikaa
 
Wataalam wa uwiano wa kuku.
Hivi kama mtu anafuga kuku 5,000-10,000,wa kienyeji au wa Kidhungu

Anahitaji kuwa na Incubator Air Force(Automatic) ya uwezo upi.
 
Uzalishaji wa vifaranga hufanyika aidha kwa njia ya asili ya kutumia kuku ama kwa kutumia egg incubators. Kwa wastani kuku 1 huatamia mayai 10 mpaka 12. Uzalishaji wa namna hii huwa na matokeo kidogo na yasiyoridhisha. Egg Incubators huzalisha vifaranga wengi kwa mda ule ule wa siku 21 na ufanisi wake ni mzuri zaidi. Kama unataka kuongeza uzalishaji wa vifaranga na kupata kipato zaidi, basi ni vema kuwa na egg incubator.
Je unaplan kuzalisha vifaranga wangapi kwa wiki na kwa mwezi? Mfano kama unaplan kuzalisha vifaranga 150 kwa wiki, basi incubator ya mayai 528 itakuwa ndio chaguo lako, maana hii kila wiki huzalisha vifaranga 176.

Kama una plan ya kuzalisha vifaranga say 300 kwa wiki, basi incubator ya mayai 1056 itakufaa zaidi kwani hii kila wiki itaweka mayai 352 na kila wiki utatotolesha vifaranga si chini ya 352 kulingana na ufanisi wa incubator na ubora wa mayai. So kama utahitaji incubator ya mayai 1056, nicheki kwenye namba hizo hapo juu. Karibuni sana.

Kuhusu umeme kukatika, inabidi uwe na backup ya generator. Generator inatakiwa at least kuwa na nguvu mara 2 ya nguvu ya incubator. Mfano kama incubator ina 200W basi generator ya kuiendesha inatakiwa kuwa na nguvu ya 500W au 600W hivi. Umeme unapokatika incubator inaweza kuhifadhi umeme kwa saa 5-6. So inabidi kuunganisha generator kabla ya masaa hayo kuisha.

Ikiwa unahitaji incubator ya mayai 528 na zaidi wasiliana nami kwa namba hizi 0783 095169, 0755 571604 na 0718 106434.
Karibuni sana!
 

Attachments

  • 1439583041637.jpg
    1439583041637.jpg
    46.3 KB · Views: 607
  • 1439583068890.jpg
    1439583068890.jpg
    79 KB · Views: 546
Kama zipo nipe bei ya hizo,nishati sola au mafuta ya taa
 
kikonko ndogo zimeisha kwa sasa tunazo za kuanzia mayai 500 mpaka 1000. Zote zinatumia umeme. Zitakapokuwepo mda sio mrefu na tutawahabarisha
 
Last edited by a moderator:
Mchanganuo mwingine ktk kuwekeza kwenye mashine za kutotolesha vifaranga. Je itarudisha gharama zako?
Hebu soma kwa makini mchanganuo huu:
Hebu tuchukulie umewekeza takribani, (2,000,000sh) kwenye mashine ya mayai 528. Utakuwa na uwezo wa kuzalisha takribani 176 vifaranga kwa wiki. Gharama zako hasa zitakuwa kwenye mayai yaliyorutubishwa na umeme. Hapo tuchukulie umekupata mayai yaliyorutubishwa kwa (400sh)@ mayai na (50sh) kama umeme utakaotumia kwa YAI, hivyo jumla ya gharama za kuzalisha kifaranga ni wastani (450sh Kifaranga. Kama utauza vifaranga vyako vyenye siku 1 kwa (1000sh) (makadirio ya haraka, inaweza kuwa zaidi), utatengeneza faida ya (550sh) @ kifaranga. Kama ukizidisha (550sh) kwa mayai 176 kwa wiki, utakuwa umetengeneza (96,800sh) kwa wiki. Sasa chukua mtaji wako uliowekeza awali wa (2,000,000sh) ugawanye kwa faida yako ya kila wiki ya (96,800sh), utarejesha gharama zako ulizowekeza awali ndani ya kipindi cha wiki 20 = miezi 5. Kama utabadilisha kidogo hizo namba hapo juu, utakuta muda mrefu kabisa utakaochukua kurejesha gharama zako za awali ulizowekeza itakuwa miezi 6. Hivyo jibu ni kati ya miezi 4 mpaka miezi 6 imechelewa sana mwaka 1 baada ya hapo ni faida tutu.
Unaweza kutengeneza kipato zaidi ya hapo kwa kufanya biashara ya kutotolesha mayai, na kuzalisha vifaranga kasha kuwalea na kuwauza kama kuku wazima. Kiukweli gharama zako zitarudi mapema zaidi na Kupata faida na faida. Be smart and make smart investment.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom