Nunua na Aliexpress: Tuelimishane manunuzi mtandaoni

Dadeki..[emoji28]

Ukitaka ufike mapema zaidi tumia wasafirishaji Kama dhl n.k ila gharama zake usinune.. halafu mbona imekuchukua muda mrefu hivyo maana najua free shipping huwa ni mwezi Sasa wewe duh! Au ndo tuseme corona..[emoji12]
Kuna mtu aliagiza mzigo Aliexpress November

Akaupata july

Wanasingizia corona
 
Yes Corona ilichangia mzigo kuchelewa. DHL bei mkasi sana wana App yao pia nilijaribu daah ni changamoto sana upande wa charges.
Sio corona wala nini
 
Siyo kwamba aliharibu hapana mkuu, Alibaba kule ni B2B na aliexpress ni B2C ,
 
Mshana mi nataka ka godoro kadogo
Ka kujaza hewa vinaitwa inflatable mattress naomba ufafanuzi wako mkuu
 
Nahitaji godoro dogo size kama yale ya wanafunzi ila kanajazwa upepo unaweza kuwa unakakunja unaenda nako popote kanagharimu bei gani?
 
Ivi brother Mshana
Je vitu vya kikamanda kama visu
Na aina flan ya kadeti na buti za kijeshi vipi ustaarabu wake katika kiagiziaa Ali x press
 
Wakuu habar za wakati
Mimi nataka kuagiza simu kupitia app ya Ali Express

Kweny upande wa payment kulikua na option ya web money na nyingine ya visa, Master card ect

Nimeiweka Master card yng ya Crdb na ku isave kwa ajili ya malipo mengine
Je ni salama?

Maana nimeona watu wakitumia M- pesa Master?
Je hii ni njia bora kuliko zingine?

Na sikuona hii option ya Mpesa Master card labda mtu anieleweshe vzr

Pia kweny shipping naona ipo ya ali express standards shipping (unavailable tracking) na Ali Express primeum (available tracking number)

Swali je Ali Express hana free shipping?
Na je vipi kuhusu izo Singapore Post mbona haipo option yke?
Naomba kueleweshwa

Maana seller karibu wote nilio waona wanatumia ali express standards shipping

Note: Mimi sijawahi kufanya hiki kitu naitaji muongozo!
 
1.AliExpress standard shipping ndio njia salama ambayo AliExpress wenyewe wanaiamini na kuitumia. Ndio maana sellers wengi wanaitumia. Percels zote zinapitia Singapore post kwa kuitumia AliExpress standard shipping.
Free shipping zipo kwa bidhaa nyingi tu ila zinachukua mda mrefu,Kama mwezi au miezi miwili kwa mzigo kufika.

Njia ya AliExpress standard shipping gharama zake ni za chini ukilinganisha na DHL,FEDEX,ARAMEX, ALIEXPRESS PREMIUM SHIPPING. AliExpress standard shipping inachukua siku 14 mpaka 21 Kama ikitokea hakuna delay yeyote i.e corrona, clearence etc.

2.Hakuna tofauti yoyote Kati ya mpesa MasterCard au Airtel MasterCard na MasterCard ya bank yoyote. AliExpress wanaitumia mfumo wa alipay kufanya malipo. Kwa hiyo unapolipia kupitia master card pesa inapelekwa alipay ili kuizuia isiende moja kwa moja kwa muuzaji mpaka utakapopokea bidhaa yako na kuthibitisha kuwa kweli umeipokea.

Kwa hiyo ni salama kabisa kulipia kupitia aliexpress kwa kutumia master card.
Kwa sababu sasa hivi Vodacom na Airtel wanazo MasterCard nakushauri uzitumie maana Haina haja ya kwenda bank kuweka pesa. Ni kwa mawakala tu ukiweka pesa basi unalipia bidhaa faster.
Chaguo ni lako.

Wakati wa kufanya malipo chagua option ya MasterCard.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…