trudie
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 3,668
- 8,745
Mtaani watu hawana jema, yaani ni mara mia wema wako ukaufanya kwa yatima sio jirani yako.Dah umenikumbusha mkasa ambao niliijiwa na lundo la wamama wa uswahilini kisa hizo pipi za kugawa bure.....nashukuru confidence yangu iliniokoa.....SIRUDII KUMPA MTOTO WA MTU KITU .....Nikitakiwa kufanya hivyo nitakwenda kwa watoto yatima
Kuna dada mmoja nilipanga nae chumba cha jirani ana mtoto mdogo rika la wangu pia miaka 4 au 5. Watoto walikuwa marafiki kiasi hata wangu anakula kwao na wake akija kwangu anakula (ingawa mama yake alimkataza so hakujua kama huwa anakula)
Kuna kipindi mtoto wangu akasafiri kwahiyo nikabaki mwenyewe, siku hyo nimelala mchana nikasikia mtoto analia muda mrefu, nikajua labda kapigwa na mama yake. Baada ya masaa mtoto hanyamazi nikaona bora nikamcheki ana shida gani.
Kumbe jioni karudi shule mama yake wala dada hawapo na mlango umefungwa. Ikabidi nikae nae kwangu hadi imefika muda inabidi niende kazini hawajarudi piga simu hawapokei na nyumbani hakuna mtu yoyote.
Nikaondoka nae kwenda nae kazini ( mgahawa) kufika kule nikampa chakula na juice akala nikapiga tena mama yake akapokea nikamtaarifu mtoto ninae kazini kwangu hapo saa 3 usiku hawajarudi ( imagine). Saa 4 usiku akarudi akampitia mwanae.
Hatukuonana kwa siku kama 4 hivi kutokana na kupishana siku hiyo ananifwata kazini akaniambia unajua toka siku ile nimetoka hapa mwanangu alilazwa, shida eti alikula chakula chenye sumu.
Nilijisikia vibaya sana aisee nikampa pole zake. Kwa hiyo alimaanisha mimi nilimpa mwanae sumu kwenye chakula. Chakula hicho hicho ambacho wateja wote hadi mimi tulikula. Tena akaongezea sio chakula alichokula shule maana tulipiga simu. Means ni chakula nilichompa mimi.
Toka siku hiyo sitaki shobo na watoto wa watu. Nimeapa hata nimkute anafanya nini nitapita kama kipofu vile.