Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
NUR YA MASJID BADAWY HAIJAACHA KUNG'ARA NA KUANGAZA
Masjid Badawy ilifikia kilele cha mafanikio yake makubwa kabisa katika miaka ya 1960.
Vuta hisia zako ni Mfungo Sita katika miaka ya 1950 mwishoni au 1960 mwanzoni.
Uko Masjid Badawy panasomwa maulid.
Katikati ya kinara amekaa Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan Bin Ameir.
Kushoto na kuliani kwake wako masheikh wa mji wa Dar es Salaam pamoja na Liwali Ahmed Saleh, Sheikh Mzee Ali Comorian, Maalim Mohamed Matar, Sheikh Ramadhani Abbas kwa kuwataja wachache pamoja na masheikh kutoka kila kona ya Dar es Salaam.
Hawa wote miaka hiyo ni vijana.
Katika wanafunzi wa Masjid Badawy miaka hiyo ni vijana wengine lakini watoto - watoto wa Mzee Mwita wa Mtaa wa Udoe na Sikukuu - Abdallah Mwita na nduguze Babu aliyekuja kuwa Engineer wa ndege, na Abdul Mwita (Medusa), watoto wa ukoo wa Bahdor, Ismail, Mohamed aliyekuja kuwa rubani wa ndege, na dada yao Maryam Shamte aliyekuja kuwa mtanganzaji wa BBC London, Maryam Zialor na mdogo wake Yusuf wote dada na kaka walikuja kuwa wafanya biashara wakubwa, watoto wa Mzee Chande Othman, Othman Chande na mdogo wake Mohamed, Othman akawa profesa wa Kemia na Mohamed mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ramadhani Rashid Madabida huyu akajakuwa mkubwa wa CCM Dar es Salaam, Alhad Omar, Adam Ahmad, Ismail Mohamed kwa kuwataja wachache.
Maulid yanaanza kwa Fatha anayopiga Maalim Matar kisha inafuatia Qur'an Tukufu halafu Sala Nabii.
Hizi zilikuwa siku nyingine.
Hakuna aliyeweza hata kwa mbali kuwaza kuwa barabara ya vumbi inayopita mbele ya Masjid Badawy itakuja kuwa barabara kubwa na mashuhuri na itapewa jina la Bi. Titi Mohamed.
Wakati huo Bi. Titi ni msichana anapigania uhuru wa Tanganyika.
Dunia inakwenda huku ikizunguka.
Hakuna aliyewaza kuwa uhuru wa Tanganyika utakuja na changamoto nyingi.
Shariff Hussein Badawy alipoondoshwa nchini mwaka wa 1963 Masjid Badawy iliendela kusomesha na kudumisha darsa lake maarufu lililokuwa likisomeshwa na Mufti Shekh Hassan bin Ameir na kuhudhuriwa na takriban masheikh wote maarufu wa mjini.
Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa pia na darsa la Alfajir baada ya sala tu Mtaa wa Mafia na Nyamwezi huku Mafia na Msimbazi.
Bibi yangu Asha bint Farijala alikuwa na nyumba yake hapo.
Hapo pia ilikuwapo nyumba ya Sheikh Hussein Juma baba yake Yahya Hussein.
Darsa hii ya Alfaji ikijaza wasomaji utadhani darsa ya mchana.
Lakini pigo kuwa lilikuja mwaka wa 1968 pale Sheikh Hassan bin Ameir alipoondolewa Tanzania Bara kwa amri ya serikali na kurejeshwa kwao Zanzibar kwa amri kuwa hataruhusiwa kukanyaga ardhi ya Tanganyika.
Sheikh Hassan hakurudi tena Tanganyika hadi alipofariki mwaka wa 1979.
Niliandika taazia katika barua za wasomaji na ikachapwa na Daily News.
Nasikitika "cutting" ya taazia hii nimepoteza
Lakini nuru ya Masjid Badawy haikuzimika hata kwa sekunde moja lau kama madras haikuwapo.
Wanafunzi wa Masjid Badawy walionekana kote na siku zote na walijulikana kwa ubingwa wao wa kusoma Qur'an.
Wanafunzi wa Shariff Hussein Badawy, Sheikh Alhad Omar na Ustadh Adam Ahmad walihuisha kumbukumbu ya mwalimu wao kila walipoonekana katika mikusanyiko ya Waislam wakisoma Qur'an au wakisomesha Qur'an katika madrasa zao.
Waislam walikuwa kila wakiwaona vijana hawa wa kheri walikuwa kwa wakati huo huo wakimuona Mwalimu wao Seyyid Hussein Badawy ingawa ilikuwa miaka mingi imepita toka atoke Tanganyika.
Lakini Allah ana njia zake za ajabu za kufanya mambo ambayo wakati mwingine akili ya binadamu inapata tabu kuamini kuwa inawezekana tena katika umri wake.
Kuna baadhi ya watu katika miaka ile waliokuwa na kumbukumbu ya Seyyid Hussein Badawy siku alipokwenda msikiti wa Kitumbini kuwaaga Waislam kuwa anarejea kwao Mombasa Kenya kwa kufukuzwa nchini.
Watu hawa bado wanakumbuka simanzi iliyowashika Waislam.
Umma mkubwa wa Waislam wakamsindikiza Seyyid Hussein Badawy hadi Masjid Badawy kumuaga kwa kukumbatiana na kuombeana dua.
Shariff Hussen Badawy baada ya miaka mingi sana kupita alirejea nchini.
Ulikuwa uvumi ulioenea kuwa Shariff Hussein yuko Dar es Salaam.
Waislam walipomuona kwa macho yao ndipo walipoamini.
Nilibahatika siku moja kukutana na Shariff Hussein nje ya Msikiti wa Ibadh baada ya yeye kurejea Tanzania nilikuwa na rafiki yangu Mtangara Kawawa mmoja wa wapenzi wa shariff na alituhadthia alivyotolewa Tanganyika mwaka wa 1963.
Shariff Hussein baada ya kurudi Tanzania amejenga chuo kikubwa Lushoto chenye wanafunzi wengi.
Kila nilipohudhuria shughuli ambayo Shariff Hussein alikuwapo nimeona mapenzi ya watu kwake.
Vijana watamzonga na kumuomba kupiganae picha.
Nina picha nyingi nimempiga Seyyid Hussein Badawy katika hafla kubwa katikati ya mji wa Dar es Salaam na nyingine pembezoni mwake.
Shariff Hussen alikuwa mwepesi sana wa kuhudhuria mialiko lakini kadri miaka ilivyokuwa ikisonga mbele na yeye akawa hawezi tena kutoka kama siku za nyuma.
Hakika Masjid Badawy nuru yake haijazimika.
PICHA:
Shariff Hussein akiwa kazungukwa na wapenzi wake ndani ya msikiti, Ismail Mohamed akisoma kasida Lamu Maulid (2007), Shariff Mwinyibaba akisoma kasida Lamu Mauid (2007), Maalim Mohamed Mattar, Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Ramadhani Abbas.