Nadhani historia ya TANU ilianzia kwenye uchaguzi uliomchagua Nyerere,....huko nyuma ni harakati zilizokuwa na changamoto nyingi sana... Ally na Abdul hawakuwa viongozi wa juu wa TANU.
Vito...
Chuo Kikuu Cha CCM kwa sababu za ajabu sana waliamini kuwa wanaweza kuanza kuandika historia ya TANU kuanzia mwaka wa 1954 na kufuta historia ya Africa Association (AA).
Matokeo yake ndiyo haya wewe upo hapa mimi nakusomesha historia ya TANU kuanzia AA mwaka wa 1929.
Balaa lake unaliona hapa JF huu mwaka wa 10 tunawajadili akina Sykes baba na wanae na mchango wao katika TAA na katika TANU.
Ukisema uanze historia ya TANU siku Nyerere amechaguliwa rais wa chama hiki kuna mengi utayakosa tena muhimu sana katika historia ya Tanganyika.
Hapo chini ni picha ya Mzee bin Sudi mmoja wa waasisi wa AA mwaka wa 1929 alifariki mwaka wa 1973.
Kubwa utakosa kujua historia ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) iliyoundwa kwa sababu maaulum na viongzi wa AA waliokuwa madarakani 1933, President Mzee bin Sudi na Secretary Kleist Sykes na wanamji wa Dar es Salaam kama Ali Jumbe Kiro.
Halikadhalika utakosa historia ya Kleist katika uongozi wake katika AA na haya kayaeleza mwenyewe katika mswada wa kitabu alioandika kabla hajafa mwaka wa 1949.
Huu mswada ni sura katika kitabu alichohariri John Iliffe. ''Modern Tanzanians,'' na mwandishi ni Aisha ''Daisy'' Sykes.
Utakosa pia historia ya Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na historia ya Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Luciano Tsere, Dr. Wilbard Mwanjisi na Dr. Michael Lugazia.
Hawa ni madaktari wazalendo na viongozi wakubwa katika TAA.
Mtafiti makini hawezi kupuuza historia hii.
Sijui wewe unazungumzia changamoto zipi labda uzieleze hapa.
Hakika Abdul na Ally hawakuwa viongozi wa juu wa TANU.
Abdul na Ally walikuwa katika wafadhili wakubwa wa TANU pamoja na Dossa Aziz na John Rupia na ndiyo maana kadi zao za TANU ni No. 2 na No. 3.
Hebu jiulize kwa nini Nyerere baada ya kuacha kazi ya ualimu alikwenda kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes ingawa Abdul alikuwa hana nafasi yauongozi katika TANU?
Hebu jiulize kwa nini Ally Sykes alichapisha kadi 1000 za kwanza za TANU kutoka mfukoni kwake?
Hebu jiulize kwa nini TANU iliwaachia Abdul, Ally na Nyerere kazi ya kuisajili TANU?
Haya niliyokueleza hapa ndiyo yaliyofanya kitabu cha Abdul Sykes kipendwe sana na watu kiasi sasa kitabu kinakwenda toleo la tano.
PICHA:
Kulia ni Kleist Abdallah Sykes na Mzee bin Sudi waasisi wa African Association na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).