Nurkovic aukubali muziki wa Simba SC

Nurkovic aukubali muziki wa Simba SC

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,509
Reaction score
68,228
Yule striker wa Kaizer Chiefs aliewafunga Simba goli mbili peke yake timu yake ikiibuka na ushindi wa magoli manne, amekisifu kikosi cha Simba SC kwa kandanda safi waliloonesha kwenye mchezo wa marudiano ambapo Simba iliibuka na ushindi wa magoli 3-0 na kukitabiria kufika mbali miaka ya mbeleni.

IMG-20210524-WA0012.jpg
 
Boko wasimpe hata mia, sehemu za kugusa yeye anapiga shuti, sehemu ya kutoa pasi yeye shuti hata goli la pili asingekuwa karibu na goli angepaisha, imagine ukaribu ule na goli bado mpira ulipiga nyavu ya juu.
 
Boko wasimpe hata mia, sehemu za kugusa yeye anapiga shuti, sehemu ya kutoa pasi yeye shuti hata goli la pili asingekuwa karibu na goli angepaisha, imagine ukaribu ule na goli bado mpira ulipiga nyavu ya juu
duh!.
 
Magazeti ya kibongobongo sio ya kuyaamini sana..utakuta tu li-mtu limeamua tu kutunga,na wala nurkovic hata hajasema..
"Simba ni timu nzuri sana, tulikuwa tunatarajia watakuja sana kwetu kwa pressure kubwa hivyo hatukuwa na lakufanya zaidi ya kujitahidi kuwazuia" - Nurkovic.
 
"Simba ni timu nzuri sana, tulikuwa tunatarajia watakuja sana kwetu kwa pressure kubwa hivyo hatukuwa na lakufanya zaidi ya kujitahidi kuwazuia" - Nurkovic.
Sikujua kumbe nurkovic anajua kiswahili?
 
Hakuna watu waongo kama waandishi wa Tanzania, utacheka wanapokutana na mtu anayeongea kiingereza au lugha nyingine tofauti na kiswahili, wanamzunguka na mic wanabaki na vigugumizi tuu akishaondoka sasa wanaanza kuandika wanayoyajua
 
Magazeti ya kibongobongo sio ya kuyaamini sana..utakuta tu li-mtu limeamua tu kutunga,na wala nurkovic hata hajasema..
Kweli aisee. Kuna mwandishi aliandika Haji Manara alizimia mara mbili kule sauzi. Kumbe ni inshu za uongo tu. Hii nchi tunaishi na tamaduni za kipekee sana.
 
Aitabiria makubwa yapi sasa wakati Simba wenyewe washaanza kutafutana uchawi hivyo kikosi kitafumuliwa
 
Yule striker wa Kaizer Chiefs aliewafunga Simba goli mbili peke yake timu yake ikiibuka na ushindi wa magoli manne, amekisifu kikosi cha Simba SC kwa kandanda safi waliloonesha kwenye mchezo wa marudiano ambapo Simba iliibuka na ushindi wa magoli 3-0 na kukitabiria kufika mbali miaka ya mbeleni.

View attachment 1796073
Utopolo watapinga
 
Back
Top Bottom