PreGE2025 Nuru Ngereja, Katibu CCM Mkoa wa Morogoro Aanza Kazi Rasmi

PreGE2025 Nuru Ngereja, Katibu CCM Mkoa wa Morogoro Aanza Kazi Rasmi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

WhatsApp Image 2025-03-26 at 18.57.18 (1).jpeg

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro, Ndugu Nuru John Ngereja ameanza majukumu yake rasmi baada ya kukabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Katibu CCM Mkoa wa Morogoro, Ndugu Solomon Kasaba

Ndugu Nuru John Ngereja amefanya zoezi la kukutana na kujitambulisha kwa viongozi mbalimbali wa Taasisi Mkoa wa Morogoro ikiwemo viongozi wa Asasi na Taasisi za Kijamii, Mashekhe na Maaskofu, Waandishi wa Habari, Makundi ya Wamachinga, Wafugaji, Mabucha, Mama Lishe, Vinyozi na Makundi ya Usafirishaji ya Daladala, Bodaboda, Bajaji, na Magari ya Mizigo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Aidha, Katibu Nuru John Ngereja ametembelea Matawi ya CCM yaliyopo kwenye Kata za Mwembesongo na Kata ya Mji Mpya kwa lengo la kufanya tathmini ya zoezi la ugawaji wa Kadi za Kielektroniki (Kidijitali) linavyoenda kwa Kadi kugawiwa kwa wananchi (wanachama wa CCM)

WhatsApp Image 2025-03-26 at 18.57.19.jpeg


Katibu Nuru John Ngereja Katika ziara hiyo, aliambatana na viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa Morogoro akiwemo Katibu Uenezi CCM (M), Ndugu Zangina S. Zangina, Katibu CCM Wilaya, Katibu Mwenezi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini na viongozi wengine
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-03-26 at 18.57.18.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-26 at 18.57.18.jpeg
    112.2 KB · Views: 30
  • WhatsApp Image 2025-03-26 at 18.57.18 (2).jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-26 at 18.57.18 (2).jpeg
    120.7 KB · Views: 32
Back
Top Bottom