Nusrat Hanje: Tanzania bado tunalima kama ilivyolimwa Eden

Nusrat Hanje: Tanzania bado tunalima kama ilivyolimwa Eden

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mbunge wa Viti Maalum, Nusrat Hanje amesema Taifa bado linalima kama Adam na Hawa walivyolima Eden. Ameeleza, "Tunalima Kilimo kinachotegemea Mvua na kudra za Mwenyezi Mungu katikati ya mabadiliko makubwa ya Sayansi na Teknolojia.

Vilevile Mbunge huyo amesema kauli ya "Kilimo ni Uti wa Mgongo wa Taifa" imepelekea Bajeti ya Wizara hiyo kutekelezwa chini ya 50% kuanzia mwaka 2016 hadi 2021.

Amefafanua, "Ipo haja ya kubadilisha kauli ya "Kilimo ni Uti wa Mgongo wa Taifa" pengine inayofanana na "Kilimo ni Oxygen ya Uchumi wa Taifa". Nafikiri kauli hii ndio inatufikisha hapa leo. Unaweza kuvunja Uti wa Mgongo ukaendelea kuishi, ila ukikosa Oxygen utakufa".
 
Kwani bustani ya Eden Adam na hawa walilima kitu gani? navyojua Mungu aliwaweka pale wakakuta kuna kila kitu, akawaruhusu wale matunda yote kasoro ya mti wa katikati, huyu Hanje anataka kutudanganya Adam na Hawa walikuwa wakulima.
 
Ametoa suluhisho la nini kifanyike au anaona kutoa maoni pekee inatosha?
Huwa wanabwabwaja tu, Mwisho wa siku wanaishia kugawana pesa na kukopeshana mamilioni, wakati huo wewe ukienda kuomba mkopo benki ya kilimo, hawakupi hadi uje na business plan, ukijitutumua na kwenda na hiyo bs plan, usubiri yesu arudi ndio upewe mkopo.
 
Kwani bustani ya Eden Adam na hawa walilima kitu gani? navyojua Mungu aliwaweka pale wakakuta kuna kila kitu, akawaruhusu wale matunda yote kasoro ya mti wa katikati, huyu Hanje anataka kutudanganya Adam na Hawa walikuwa wakulima.
Hahaha! Ndivyo watu wanavyoisoma Biblia kuwa Adam na Hawa walikuwa wamewekewa kila kitu? Ina maaana hata Sungura walikuwa wanawindiwa na kuchinjiwa? Hata huyo Nusrat amejenga hoja ya kijinga tu.

Yeye anajuaje kuwa jamii ya Mwanzo(Adam na Hawa) hawakuwa wanatumia Kilimo cha Umwagiliaji? Kwani wakati huo hakukuwa na Maji ili kuruhusu Umwagiliaji?
 
Kwani bustani ya Eden Adam na hawa walilima kitu gani? navyojua Mungu aliwaweka pale wakakuta kuna kila kitu, akawaruhusu wale matunda yote kasoro ya mti wa katikati, huyu Hanje anataka kutudanganya Adam na Hawa walikuwa wakulima.
Kasome Mwanzo 2:15
 
Kusema tu kuwa ni Mbunge haitoshi, bali ni mbunge binafsi (Private MP). 😹😹 kwa kweli, Bongo sihamii!!
 
Back
Top Bottom