Nusu Fainali ya Azam Sports Federation Cup, Yanga SC dhidi ya Simba SC kupigwa CCM Kirumba

Nusu Fainali ya Azam Sports Federation Cup, Yanga SC dhidi ya Simba SC kupigwa CCM Kirumba

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya michuano ya Azam Sports Federation Cup hatua ya Nusu Fainali kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC, inatarajiwa kupigwa Jumamosi ya Mei 28, 2022 majira ya saa 9:30 Alasiri, kwenye Dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Nusu Fainali ya pili itapigwa Jumapili ya Mei 29, 2022 majira ya saa 9: 30 Alasiri kwenye Dimba la Sheikh Amri Abeid Mjini Arusha, ikiikutaniasha Azam FC dhidi ya Coastal Union.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Tanzania (TFF) imetoa ratiba hiyo leo Mei 16, 2022
View attachment 2226863
 
Patashika ya michuano ya Azam Sports Federation Cup hatua ya Nusu Fainali kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC, inatarajiwa kupigwa Jumamosi ya Mei 28, 2022 majira ya saa 9:30 Alasiri, kwenye Dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza...
Jee, hiyo itakuwa marudio ya yaliyojiri mwaka 1974 hapo CCM Kirumba kati ya timu hizo mbili?
 
Askari wa wanayapori wajiandae tu kutukamata aisee! Siku hiyo lazima tumtafune mnyama. Ubingwa pasipo kula nyama ya porini haunogi hata kidogo.
 
Historia Ni muhimu Sana.
Okay, nimekumbuka Simba kwenye michuano hii ana historia ya kupiga mabao kuanzia 1 hadi 7

Kwahivyo kuna ambaye anakula nyingi siku hiyo.
 
Okay, nimekumbuka Simba kwenye michuano hii ana historia ya kupiga mabao kuanzia 1 hadi 7

Kwahivyo kuna ambaye anakula nyingi siku hiyo.
Wewe subiri hiyo siku Historia iwachinje, maana ili kombe ndu mmelitolea macho
 
Mpaka hapo simba mwaka huu tumemaliza na kombe la mapinduzi tu [emoji22][emoji22][emoji22] so sad!
Simba hawezi fungwa na vipofu kama utopolo. Timu ambayo mechi iliyoisha haikulenga lango la simba hata mara Moja.

Linapokuja suala la fainali , nusu fainali , robo fainali dhidi ya utopolo simba huwa hafanyi makosa. Tunza hii comment .
 
Simba hana timu ya kunfunga Yanga zaidi ya uchawi na kuhonga waamuzi.
 
Mapema kabisa nakwea Ally's Dar to Rock City nikaone mnyama anavyo mvua chupi dada wa kijani na njano.
 
Back
Top Bottom