Mleta mada ANAPOTOSHA tafsiri ya hiyo takwimu...nianze kwa kusema ni kweli imekuwa published kuwa 44% ya watoto ambao wanaenda kufanya kipimo cha vinasaba (DNA) kwenye ofisi ya mkemia mkuu imethibitika sio wao (baba). Lakini hii haina maana kuwa kati ya watoto wote wa kiTanzania karibu nusu sio wa baba wanaoishi nao...hii ni 'mis-interpretation' ya hiyo takwimu.
Hapa Tanzania, kipimo cha DNA kutambua mzazi halisi wa mtoto, hufanyika kwa maombi maalum toka 'Mahakamani' ambapo huwa na kesi ya kutambua mzazi halisi wa mtoto, kwa hiyo tayari umeshasegment sample yako kwa watu ambao kwa sababu moja au nyingine hawaamini kuwa ni baba halisi wa watoto hao...tayari hapo kuna mazingira ya kutoaminiana, na hivyo takwimu hii tayari iko biased na huwezi kuigeneralize kwa population nzima ya watoto wa kiTanzania....kosa ambalo mleta mada umelifanya.
Ili kuweza kugeneralize takwimu ili kurepresent general population, itabidi ufanye sampling kwa kutumia techniques sahihi za sampling kupata kweli sample size inayorepresent general population kuweza kugeneralize results zako. Kwa hiyo iwapo ofisi ya mkemia mkuu, wangechagua population sample ya watoto kwa ukubwa unaoshauriwa na kuwapima vinasaba, then hapo waweza sema asilimia 44% ya watoto wa kiTanzania...in short of that, NO!