Nusu ya wanaume Ulaya hawafui mashuka yao. Just Imagine Tanzania hali itakuaje?

Nusu ya wanaume Ulaya hawafui mashuka yao. Just Imagine Tanzania hali itakuaje?

Unakuta kijana wa kiume boxer akiivua akiiweka chini inasimama wima kwa kukakamaa kwa uchafu..........boxer inaweza kumaliza ndoo nne za maji maana kila akiisuuza bado inabadilisha rangi ya maji.......watu tumetofautiana sana....
 
Em acheni kutunanga wanaume aisee.

Sio kwamba ni uchafu, sasa kitu hakijachafuka kwanini ukisafishe??

Mtu hujachafuka, hujafanya kazi ngumu ya kukutoa jasho siku nzima then usiku mwanaume kabisa eti unaoga unaogopa kulala bila kuoga nyambafu kabisa.

Wanawake ndio wanaotakiwa kuoga mara kwa mara kwasababu ya maumbile yao na wasipooga kiukweli huwa wanatoa harufu. Lakini wanaume asilimia kubwa mpaka atoe harufu huyo mwamba ajue kavuta wiki/ wiki na siku kadhaa mwili hauyajui maji.

Lakini hizi desh za siku tatu/nne wala sio big deal.

NB: kufua shuka inategemeana na rangi yake, kila rangi ina muda wa kufuliwa.
Mwanume unaejielewa huwez kununua shuka jeupe na hujaoa, utakua umezingua sana.( Labda ununue kwa matukio maalumu na tukio likiisha hakikisha unalitoa haraka sana.)
 
Hivi kuna watu wanafua mashuka na hamsemi?
Dunia ina watu wasiri sana
 
Wengine hufua kwa installments.nguo,mashuka,neti nk hufuliwa kwa installments nne kwa mwaka mzima...
 
Aki kuna binadamu n wachafuu, nmeshuhudia watu hao. Mwanaume boxer anayo moja tu n kuirudia tuu, mdgo wangu alianza hiyo tabia nlimnyoosha.

Sasa hv ana boxer zaid ya 10 na anazngatia usafi, maana nlimuambia usafi n wa kila mtu s wa watt wakike tuu.
Aiseee swala la uchafu sio kabisa.
 
Mmepata wapi uhalali wa kusema wanaume wote hawafui mashuka kwa ka utafit kadogo ka hapo kwa malkia?mimi kila baada ya siku tatu nafua shuka regardless nnepiga mshariboko au laha!
 
Wazungu wachafu Sana,

mtu ambae anaona kastaarabika sana kuchamba kinyesi kwa karatasi (tissue) badala ya maji.


Unamshangaaje Sasa anapokaa miez 4 Bila kufua mashuka.

Usikute huo nao Ni ustaarabu ulaya,
Huku afrika labda ndio ushamba wetu tu
Kati ya vitu vilivyonishinda ni kutumia tissue halafu nibaki comfortable.

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
 
Hata kuoga pia hawaogi.
Zaidi ya kunawa uso na kujiosha kwenye makwapa.

[emoji3][emoji3].
 
Back
Top Bottom