kimbendengu
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 8,394
- 16,128
TUNAENDELEA KUPELEKA BARUA HAPO FIFA BAADA YA YANGA KUTOA BILIONI 10 KWA CCM
Naona anawajibia ccm kama mwenezi wa chama. Kazi ipoView attachment 3440183
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty amesema Sheria ya Gharama za Uchaguzi haijaweka ukomo wa kuchangia fedha za uchaguzi na kwamba sio lazima fedha walizochangisha CCM zote zitumike kwenye uchaguzi.
Kauli ya Nyahoza imekuja ikiwa ni siku moja tangu CCM walipochangisha Zaidi ya Sh86.31 bilioni katika harambee iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Agosti 12, 2025 zikiwa ni sehemu ya Sh100 bilioni zinazokusudiwa kukusanywa kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Akizungumzia michango hiyo leo Agosti, Nyahoza amesema Sheria ya Gharama za Uchaguzi haijaweka ukomo.
“Hakuna ukomo, wanaweza kuchangisha tu. Ni kama CHADEMA walivyokuwa wanachangisha Tone Tone, kwani kuna wakati walisema zimetosha?”
Alipoulizwa kuhusu kikomo katika matumizi katika uchaguzi, Nyahoza amesema wanaohoji uchangishaji wa fedha za uchaguzi uliofanywa na CCM, wanatumia nyaraka zilizopitwa na wakati.
Nyahoza ametaja kipeperushi kilichotolewa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa chenye kichwa: “Ijue Sheria ya Gharama za Uchaguzi; Ukomo wa Gharama za Uchaguzi”, akisema kimepitwa na wakati.
“Kwa sasa kuna sheria mpya iliyotoka wiki mbili zilizopita, ingia kwenye website yetu utaona. Hicho kipeperushi kimepitwa na wakati,” Nyahoza amemwambia mwandishi aliyemuuliza kuhusu kipeperushi hicho.
Katika Kipeperushi hicho, kuhusu ukomo wa matumizi, kifungu cha 2 kimesema, Ukomo wa gharama za uchaguzi kwa chama cha siasa katika kampeni za uchaguziu ni shilingi bilioni 17. (3) Ukomo wa gharama za uchaguzi kwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni shilingi bilioni 6.”
Alipoulizwa kuhusu fedha za CCM, Nyahoza amesema, “Sio lazima fedha zote zikatumike kwenye uchaguzi, zinaweza kutumika kwenye matumizi mengine ya chama. Hata wenyewe walisema kwamba sio fedha zote zitatumika kwenye uchaguzi.”
Stupid, stupid, stupid. Kumbe wewe mpuuzi, unawatetea CCM. Ulaaniwe!View attachment 3440183

Tutazifanyia Kazi Pale Zitakapowasilishwa Kwa Umma....Sheria mpya sa hizi zinatungwa nyingi mno za kuibeba CCM na serikali
Kuna Sheria mpya inakuja ya kuzuia kauli na misimamo ya NRNE
Kweli haya ni maigizo kama mengine.Samia hakubaliki sio tu kwa wananchi hadi kwa ccm wenzake, ndio maana kila siku yeye na baadhi ya viongozi wana kuja na matukio kuonyesha watu na mataifa kuwa ana kubalika.
Bil86 kuchangiwa ilikuwa ni kiini macho, ccm itakuwa imekwapua pesa already kutoka serikalini na kutumia kiini macho cha jana, na kuwapa taarifa wafanya biashara wewe taja kiasi hiki cha pesa mbele ya watu na camera zikuone.
Kumbuka alikuja na kiini macho kingine cha kugawa baiskeli, na kiini macho kingine kina kuja cha kugawa mifuko ya Samia hehe hili ni janga taifa.
Lakini ukijiuliza anafanya haya yote ili iweje? Kushindana na Salum Mwalimu, Mpina au John cheyo?, ni ujinga mtupu anachofanya kuwaaminisha watanzania na jumuiya za kimataifa kuwa ana kubalika sana na kuna demokrasia.
Watanzania ndo watu wajinga, ambao wamekubali, kwahiyo acha wapigwe na maigizo ya Samia.