PostGE2025 Nyahoza: Tumeiandikia barua CCM kauli za Chatanda

PostGE2025 Nyahoza: Tumeiandikia barua CCM kauli za Chatanda

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
Siku mbili baada ya Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Taifa, Mary Chatanda kusema akipewa dakika moja awe Rais atawafuta wapinzani, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imekiandikia chama hicho barua ya kujieleza.

Sisty Nyahoza.jpg

​
Chatanda alitoa kauli hizo Mei 18, 2026 mkoani Iringa wakati wa kampeni za kumnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho, katika Jimbo la Isimani, Emmanuela Mtatifikolo, anayewania nafasi iliyoachwa wazi kufautia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, William Lukuvi.

1779344183006.png

Alisema; “Nasema, kama ningekabidhiwa nchi hii hata kwa dakika moja tu! Mama Samia, sijui kama wale watu wangekuwepo. Wamemkuta ndugu yetu mpendwa, Dk Samia, akiwa mpole, mnyenyekevu na msikivu.

“Wakisema jambo, anawasikiliza; mara amewafungulia waliokuwa jela, mara ameenda kunywa nao chai kule Ikulu, halafu wanarudi tena kumtukana. Mimi nisingeweza,” alisema.

Kauli hiyo imezua mijadala miongoni mwa wananchi ikitajwa kuchochea chuki za kisiasa.

Soma: Mary Chatanda: Samia angenipa nchi dakika moja, ningeimaliza CHADEMA

Akizungumza na gazeti la Mwananchi Mei 20, 2026, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, amesema ofisi yake imezipokea video na taarifa za matamshi hayo na tayari imechukua hatua.

“Kuhusu suala la Mheshimiwa Chatanda, nasi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa tumetumiwa video na picha hizo, na tumekwisha kuiandikia CCM barua ili wawasilishe maelezo kuhusu suala hilo,” amesema Nyahoza.
 
Amewaambia wajieleze kwanini chama chao kisifutwe/kusimamishwa au amejitongozesha tuu kwa mabosi wake?
 
Chatanda mwenyewe ni very ugly kama roho yake.
 
Nakumbuka kuna siku jeshi la polisi "lilizuia" maandamano ya CCM 😂 😂 😂 😂
 
Hahaha. Anamdanganya nani huyu?
Angetueleza kwanza kwa miaka yake yoote ofsini aliwandikia ccm bartua ngapi? Hivi anaikumbuka kauli ya makala dhidi ya virusi huyu?
 
Kuhusu suala la Mheshimiwa Chatanda, nasi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa tumetumiwa video na picha hizo,

Huu ni ujumbe wa kunyenyekea mhalifu
 
Back
Top Bottom