DMmasi
JF-Expert Member
- Nov 28, 2020
- 561
- 900
Habari Wanajamvi,
Naona utandawazi unatupeleka kwenye mambo ya "daddy it's my right" au "mama, nataka kuondoka nyumbani."
Kwa sasa, mzazi anapata kesi kwa kumuadhibu mtoto! Leo nawakumbusha aina za vichapo tulivyokuwa navyo:
Hali hii inamfanya mtoto aishi kwa huzuni na hata kufanyiwa mzaha na wenzake, jambo linalomwathiri kisaikolojia.
Mtoto asinyimwe fimbo pale inapohitajika, lakini mzazi anayempiga mtoto kila siku, hapo shida si mtoto, ni mzazi mwenyewe.
Kichapo gani kingine unakijua? Au kipi kati ya hivi umewahi kukutana nacho?

- Kichapo Chenye Maandalizi
Hiki ni kile ambacho mzazi anapanga kabla. Mtoto anapokosea, mzazi anamwambia "Nitakuchapa jioni," na hivyo anapewa muda wa kujiandaa. Hii hufuatiwa na maneno ya lawama na maonyo, kama vile kumweleza kosa lake kabla ya adhabu. - Kichapo cha Kushtukiza
Hapa mtoto anachapwa na chochote kilicho karibu. Unaweza kukumbuka ulivyopigwa na lapa kama mende, au labda sahani, fagio, ngumi, mateke, au kwa mzazi mkorofi, hata kabati linaweza kurushwa! - Kichapo cha Makubaliano
Hiki ni kile ambacho mzazi anakusimamisha na kukuambia utafute fimbo inayokutosha mwenyewe ili upate kipigo. - Kichapo cha Kikatili
Hii ni hali ambapo mtoto anachapwa kama gaidi. Wapo wazazi wanaweza kumchoma mtoto mikono kwa sababu ndogo kama kudokoa chakula, kumwaga maji ya moto, na mengine yenye mateso makali. (Hii mimi siungi mkono hata kidogo.) - Kichapo cha Mbuzi wa Kafara
Hiki ni pale mtoto anapokutana na hasira za mambo ambayo hayamhusu. Mzazi anashusha hasira za masuala mengine kama kukosa marejesho, sponsor kasusa, au ugomvi na mzazi mwenza.