Nyakati zinabadilika. Ugumu wa maisha uko kotekote mjini na vijijini

Nyakati zinabadilika. Ugumu wa maisha uko kotekote mjini na vijijini

OgaBoy

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
4,031
Reaction score
6,156
Kipindi tuko watoto ukienda kumtembelea mjomba, shangazi, bibi na babu n.k

Utachinjiwa jogoo au mbuzi na hapo utaenjoy kama ni kijijini basi maziwa na nyama, samaki na ugali mkubwa Kisha mnashushia wali kwa kwenda mbele, kama ni mjini utakula pilau nyama na soda au juice safi ya matunda.

Na wakati wa kurudi ulikotoka utapewa mizigo ya nafaka, ndege wanyama na kama ni mjini utapewa nauli HATA kama unayo.

Utu uzima aujua Mshana Jr mambo yamekuwa magumu sio mjini sio kijijini hivi vitu kuvipata ni MPAKA uwe mtoaji KWENYE koo YAKO.

Ukienda hauna ule mvuto WA kipekee kama umekuta ugali misumari unaunga tela, kama HUNA nauli utajijua.

Unaweza weka miadi na MTU akasema yupo ukagika ndani muda mfupi unaona anajiamdaavanasema anaenda KWENYE kikoba lahaula.

Aachi HATA bia mezani ukiwa unasubiri inabidi na wewe utokee UENDE pub akirudi mnameet huko.

Sasa tuna experience ukubwa au umasikini au mambo yamebadilika.

Enewei Yanga katupa PESA wazee WA kubeti kula Bata hilo kama Jana ulienda na pupa subiri penaduu.

Akumbukwe Pdidy
 
Hata shuleni, ukifaulu kwenda sekondari ilikuwa unachinjiwa ng'ombe kabisa! Ukirudi likizo unachinjiwa mbuzi, ukirudi shuleni unaondoka na kuku wa kuoka wa kula safarini. Siku hizi hakuna uroda huo na wala jamii haisisimki hata ukipata one ya saba!
 
Nakumbuka form 4 niliokota one ya kuunga unga.
Wakati naenda kumuaga mama mdogo naenda form 5 akaniwekea kuku wa kuoka wa kula safarini.
That was when div one had real value. Kupata hiyo kitu ilikuwa kazi ngumu sana.
Mtaani kwenu au wa huko vijijini Kijiji chote na vya jirani unaheshimika hadi na wazee.
Majirani wanatamani uoe binti zao.
 
Nazan mambo yamebadlik sana,
Kwanza si kijiji si mjini ni kama iwiano wa ugumu wa maisha unaendana (bei za vyakula na bidhaa )
Maisha ya sasa kila ktu pesa
Ukilma.na kufuga lazima ununue dawa na vyakula (zaman asili ilikuw inaweza jimudu)
Kisamvu , mchicha bwasi viazi mihogo mahindi tembele nazi si tabu sana Enzi za 2000 kurud nyuma

Tumejikuta karne ambayo pato moja dogo lakin matumiz ni 100
Umeme juu
Bill ya maji
Michango ya shule
Wategezi wa karbu wakiumwa Magonjwa yalioshindikan
 
Ukiona maisha yameaanza kuwa magumu ndipo akili itaanza kukirudia. Utaacha kuamini waganga, uchawi, mungu, shetani, majini, mapepo na vitu vingine kama hivyo. Hapo ndipo utaanza kukumiza akili yako Ili kujikwamua.

Wenzetu wa kwenye mataifa yaliyoendelea walishapitia hayo.
 
Back
Top Bottom