Nyalandu asitukanwe, kazi aliyoifanya CHADEMA inatosha

Hawa jamaa (Lazaro Nyalandu & Seleman Mathew) wamenifurahisha kwa jambo moja kubwa...

Speech zao za kuachana na CHADEMA na kujiunga tena (rejoin) CCM ni za kistaarabu sana, hazina matusi...

Ingekuwa nyakati za CCM ya Mwendazake, Polepole na Bashiru, ikatokea wamefanya usajili kama huu, basi mtu asingeshangaa kumuona Mwenyekiti wa CCM taifa akichagiza wahamiaji hawa kwenye hotuba zao kumtukana matusi mazitozito Ndg. Freeman Mbowe - M/kiti CHADEMA - Taifa mwanzo mwisho huku wajumbe wakikenua meno na kucheka kama majuha kufurahia ufirauni huo...!

Ila kwa leo, binafsi wala sina tatizo kwa watu hawa kuhama chama cha siasa hiki kujisajili chama kingine hata kama kurudi mara mbili au tatu..

Na kiukweli, siasa ni Utumishi, ajira na fursa pia. Kama hupati fursa kwenye chama A, nenda chama B au hata C...

Tunawatakia kila la kheri Nyalandu na Mathew pamoja na wengine wanaojiandaa kutoka CCM kwenda CHADEMA au CHADEMA kwenda CCM...
 
Kama vile kuna kaukweliiii
 
Akitaka asitukanwe basi aache kashfa ,sasa mambo ya wimbo haumbiki yametoka wapi? Ushasikia ENL ametukanwa alipotoka CDM? Ukihama kimya kimya hakuna atayesumbuana na wewe.
 
Ukweli ni kwamba , Nyalandu alilikimbia dicteta na matendo ya dicteta kule CCM. Ni haki yake kurudi nyumbani
 
Na pia tuelewe , ndani ya miaka Mia ijayo wote tuliopo hai leo tutakuwa maiti , hata hvyo Tanzania itakuwepo ikichanja mbunga , sometime inabd utazame hatima yako , kuliko kuwaangalia wananchi wenye akili za darasa la saba
Miaka 100 kote huko mbona mingi, kuna wengine wana 70 ....
 
Ukweli ni kwamba , Nyalandu alilikimbia dicteta na matendo ya dicteta kule CCM. Ni haki yake kurudi nyumbani
Jiwe hakuwa na urafiki na wezi na ndio maana walikuwa wanakimbia ,mwambieni arudishe twiga wetu.
 
Ujumbe muhimu sana hususani kwa viongozi au makada maarufu ndani na nje ya cdm....tuwape heshima yao, tusijishushie weledi mbele ya jamii. Tukiwasikua watukanaji na wakosaji wa vijiweni wakiwananga haina madhara sana km kwa viongozi na makada kindakindaki. Tujifunze kuona mema, wema na kushukuru
 
Mjinga ni wewe unayeabudu mlewa konyagi Dj mwenyekiti wa milele unayedhani ipo siku atakutoa kwenye lindi la umasikini ulionao
 
Nimekuelewa sana mkuu
 
Acha kulinganisha dr. Slaa na vitu vya kijingakijinga
 
THANK YOU! πŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎ
What so ever "political prostution is un ecceptable in a modern world" he is apolitical opportunist
 
Huko alikua jehanamu


πŸ‡¦πŸ‡·πŸ‡¦πŸ‡·πŸ‡¦πŸ‡·πŸ”₯πŸ”₯
 
Siasa ni kazi kama kazi nyingine..

Mbowe anastahimili kwenye siasa kwanza kwasababu Ukoo wake especially Baba yake tayari walishaanza kutengeneza pesa tangia miaka ya 50..

Lakini Pili sababu matajiri wengi wa Kichaga wanadhani Utawala wa CCM unawakandamiza hivyo kutamani mtu/chama chenye mlengo wa kabila lao kitachukua madaraka hivyo kukisaidia CDM kichukue nchi na wao wapate ahueni/faida fulani..

Siasa ni biashara.. Hakuna mtu atasimama jukwaani akupigie kelele wewe alafu yeye asipate chochote. HAKUNA
 
Asantd technically kwa maoni yako na yataheshimiwa kwa sababu ni maoni yako.
Hebu weka kumbukumbu sawa;
Unakumbuka wakati Nyalandu anahama CCM maneno yaliyosemwa na makada wa CCM si mitandaoni pekee bali hata kwenye majukwaa ya kisiasa?
1.Aliiba Twiga akapakia kwenye ndege na kulazimisha kukunja shingo yake ili asionekane.
2.Aliiba fedha za wafadhili walizotoa kutangaza utalii akenda kula bata na demu wake (Mi namwita mke) Faraja Kota.
3.Aliuza vitalu vya uwindani kwa bei ya bustani ya nyanya.
4.Alipishana angani na bosi wake Kikwete kama Kunguru na Mwewe kwa safari za nje ya nchi.

Hayo na mengine ya nguoni yalisemwa na ambao Jana walimshangilia sana na wengine wakiwa wasemaji wakubwa wa Chama alichorejea.

Maneno machache makali uliyoyaona humu ni kutokana na hotuba yake fupi ya Jana iliyojaa mafumbo toka Biblia Takatifu kitabu cha Zaburi ya Daudi.
Machache yanayokera;
1.Walituteka - Nyalandu alitekwa na CHADEMA.
2.Walitaka tuwaimbie nyimbo za Sayuni - Akimaanisha walitaka awape siri za CCM. Kwa maana nyingine Nyalandu ana siri za CCM ambazo zingekuwa faida kwa CDM, kwa akili ya kawaida zipo?
3.Tutaimbaje wimbo wa Bwana katika nchi ya ugenini? - Nini kilimpeleka CDM kama CCM ilikuwa sehemu sahihi kwake kwa kipindi husika? Kama watu walikupa hifadhi katika kipindi cha dhiki yako kwa nini uwaage kwa kuwasimanga?
4.Tulilia tulipokumbuka Sayuni Mji wa Baba - Hapa aliwataja aliolia nao akiwa ugenini ambao ni Lowasa akamtafuta Jana kama yupo hakumwona, akamwita Sumaye Baba nakuona pale, akamwita Dr Slaa. Anaongea akimaanisha walinyanyaswa na viongozi wakiowakuta/waliowapokea. Tafsiri nyepesi ni kwamba walinyimwa vyeo walivyogombea. Tuchukue uhalisia, Lowasa alijiunga na kupewa kugonbea Urais, Sumaye alipewa Uenyekiti wa kanda ya Pwani lakini akashindwa Uenyekiti wa Taifa, Yeye alipewa Uenyekiti kanda ya Kati na kugonbea Ubunge akanyimwa kugombea Urais. Je, kilichowapeleka huko ni kujenga walichokikuta au kupewa wasichokijenga? Yaani walitaka wapate kila walichotaka mbona huko walikokuwa hawakuwahi kupata kila kitu mbali ya wote kuwahi kuomba kuwa Wagombea Urais? Anamaanisha wao ni " The winner takes all?"

Mara zote nasimama na ukweli, namheshimu Nyalandu kama ninavyowaheshimu wanasiasa wote wanaojua maana ya utu ambapo ndani ya CCM wako wachache sana. Lakini maneno yake ya kuaga Jana hakuyachagua vizuri na kama ana nafasi arudi aseme upya maneno yasiyowananga waliomhifadhi wakati wa shida. Wakati ambapo hakuwa na pa kushika, wakati ambapo hakuwa na kinga, wakati ambapo hakuwa na rafiki, wakati ambapo hakuwa na NAFASI akapewa uwanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…