Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri wa zamani, Lazaro Nyalandu, amewasihi viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Hanang mkoani Manyara kuhakikisha mipango inafanyika ili watu wenye ulemavu na wazee waweze kufika kwenye vituo vya kupiga kura.
Nyalandu ametoa kauli hiyo jana Septemba 16, 2025 katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Gehandu, ikiwa ni kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025. Amesema ni wajibu wa vijana na viongozi kusaidia wasioweza kufika kwa urahisi kwenye vituo vya kupigia kura.
"Tunapita kuwaomba vijana kuwasaidia wazee na wenye ulemavu na waliopo mbali ili wafike kwenye vituo vya kupiga kura," amesema Nyalandu.
Nyalandu anaongoza kampeni za kumtafutia kura mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan, kupitia kampeni yake ya ‘Samia Love’, akisisitiza umuhimu wa kila mmoja kushiriki mchakato wa uchaguzi.